Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, September 1, 2013

ALICIA K DESIGNS YAANDAA USIKU WAJASIRIAMALI WANAWAKE


 Mbunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Shrose Bhanji akizungumza kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Alicia K Designs kwa ajili ya kuwapa wanawake mbinu za ujasiriamali katika ukumbi wa Mezaluna jijini Arusha.
 Mbunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Shyrose Bhanji (wa pili kulia) akiwasha Mshumaa, ishara ya upendo wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Alicia K Designs. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Alicia Matasia, Mwanamitindo ambaye ni mke wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Faraja Kota Nyalandu na Mjasiriamali wa jijini Arusha, Isabela Mwampamba.
 Mbunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Shyrose Bhanji (wa pili kulia) na Mwanamitindo, Faraja Kota Nyalandu wakikata Keki wakati hafla ya Chakula cha jioni,iliyofanyika Mezaluna jijini Arusha.
 Mbunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Shyrose Bhanji (wa pili kulia) akimlisha Keki Mjasiriamali wa jijini Arusha, Isabela Mwampamba wakati wa hafla ya usiku iliyoandaliwa na Alicia K Designs, shoto ni Mkurugenzi wa taasisi hiyo,Alicia Matasia na Mwanamitindo, Faraja Kota Nyalandu
 Burudani ya nguvu ilikuwepo kuwafanya wasichana na wanawake waliohudhuria kuburudika vilivyo.
Mkurugenzi wa Alicia K Designs, Alicia Matasia akitoa neno la shukrani kwa wageni waliofika kwenye hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...