Kiungo mshambuliaji mpya wa Real Madrid, Gareth Bale
ameanza kukutana na joto ya jiwe klabuni hapo baada ya Kocha msaizidi wa timu
hiyo, Zinedine Zidane kutokubali usajili ghari wa mchezaji huyo.
Mkongwe huyo ambaye aliwahi kuichezea klabu hiyo
alisema jana kuwa hakubaliani ya mchezaji huyo kutoka Tottenham Hotspur kusajiliwa
kwa dau kubwa la pauni 85.3 milioni kwani kiwango chake hakiendani na fedha
hizo.
Bale, 24, alijiunga na Madrid Septemba mosi na
kuvunja rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwa fedha nyingi rekodi
iliyokuwa ikishindikiwa na Cristiano Ronaldo aliyesajiliwa na klabu hiyo
akitokea Manchester United mwaka 2009 kwa ada ya uhaimsho ya pauni 80 milioni.
"Miaka 10 iliyopita nilinunuliwa kwa pauni 48
milioni na nilisema kuwa sikustahili kununuliwa kwa fedha hizo," alisema Zidane.
"Sasa nafikiria pia kuwa mchezaji hawezi kustahili kununuliwa kwa kiasi
hicho cha pesa. Huu ni mpira wa miguu, sielewi nini kinatokea hadi mchezaji
ananunuliwa kwa fedha nyingi kiasi hicho."
No comments:
Post a Comment