Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, September 9, 2013

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AWASILI NZEGA, APOKEA PIKIPIKI 9 KUTOKA KWA DK. KHAMIS KIGWANGALA NA KUKABIDHI KWA KATA 9 ZA CCM


1Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Siasa Ndugu Nape Mosses Nnauye ukiwasili katika mji wa Nzega Katika wilaya hiyo Tayari kwa kuanza Ziara ya Siku 18 katikia mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara kesho ambapo ziara hiyo itaanza katika mkoa wa Shinyanga, Katibu Mkuu huyo amepokelewa na viongozi mbalimbali wa chama na wananchi waliojitokeza katika mapokezi hayo, Kinana leo amezungumza na wananchi wa Nzega na kukutana na vikundi mbalimbali vya ujasiriamali ambapo pia amepokea Pikipiki tisa kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo Dk. Khamis Kigwangala ambazo ambazo amezikabidhi kwa viongozi wa kata 9 kati ya 21 zilizopo katika Wilaya hiyo, ambapo pia amekabidhi mashine ya kutotolea vifaranga vya kuku kwa kikundi cha wazee wa Nzega , Pikipiki hizo zimekabidhiwa katika kata za Budushi, Ndala, Puge, Nkininziwa,Mbogwe, Lusu, ,Ijaniga, Utwigu na Isanzu baadae pikipiki 7 zitafutaiwa na kisha kata tano za mwisho. PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-NZEGA 2Vijana waendesha pikipiki na baiskeli wakiongoza msafara wa Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 3 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa skafu mara baada ya kuwasili wilayani Nzega leo 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipita katikati ya vijana wa Greenguard wa CCM huku wakitoa heshima zao mble ya mgeni huyo mara baada ya kuwasili wilayani Nzega leo. 5Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali. 6 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanachama mbalimbali na wananchi mara baada ya kuwasili wilayani Nzega. 7Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi 8 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisamewa risala wakati alipozindua mradi wa ujenzi wa vibanda vya biashara vya mradi wa Chama cha Mapinduzi Wilayani Nzega. 9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa ujenzi wa vibanda vya biashara katika uwanja wa Samora, vibanda hivyo ni mradi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilayani Nzega. 10Mbunge wa Jimbo la Nzega Khamis Kigwangala akizungumza na wananchi huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza. 11Katibu wa Itikadi, Uenezi na Siasa Ndugu Nape Mosses Nnauye huku katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipiga makofi 12 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi huku Mbunge wa Jimbo la Nzega Khamis Kigwangala akimsikiliza. 13Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika mapokezi hayo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...