Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahamani Kinana akiongozwa na Mkuu wa Moa wa
Singida Dk, Parseko Kone, Katibu Tawala Lianna Hassan na viongozi
wengine wa Mkoa wa Singida kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa
hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, wakati Kinana alipokuwa Mkoani
Singida kwa ziara ya kikazi ya siku saba.(Picha na Zainul Mzige
wa modewjiblog).
Na Nathaniel Limu, Singida
MKUU
wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone amesema serikali imetoa zaidi
ya shilingi 6.7 bilioni kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa hospitali ya
rufaa ya mkoani hapa iliyoko kijiji cha Madewa nje kidogo ya Singida
mjini.
Dk.Kone amesema hospitali hiyo itakapokamilika,itahudumia wagonjwa kutoka mikoa yote ya kanda ya kati.
Mkuu
huyo alitoa rai hiyo wakati akitoa akitoa taarifa yake kwa katibu mkuu
CCM taifa,Abrahamani Kinana aliyetembelea hospitali hiyo hivi karibuni.
Amesema
mkoa umetegewa eneo la ekari 283 kwa ajili ya uendelezaji wa mradi wa
hospitali hiyo, ambayo itakuwa ya mfano hapa nchini.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Dorothy Gwajima amesema
lengo la mradi huo ni kuimarisha huduma za afya mkoani pamoja na mikoa
jirani.
Katibu
Mkuu wa CCM akiweka saini kwenye kitabu cha hospitali ya Rufaa huku
Naibu Katibu Mkuu wake Mwigulu Nchemba na mkuu wa Mkoa wa Singida Kone
wakishuhudia.
Dk.Gwajima amesema mradi huo utakapomalizika,utakuwa na majengo 29 yatakayotumika kutoa huduma mbali mbali.
Mganga
huyo mkuu,amesema changamoto inayowakabili ni pamoja na uhaba wa
watumishi,nyumba za kuishi watumishi na ufinyu mdogo wa bajeti ya dawa
kutoka bohari kuu ya madawa (MSD).
Kwa
upande wake Kinana,alitumia fursa hiyo kumpongeza Dk.Kone kwa utendaji
kazi wake ambao umesaidia kujengwa kwa hospitali hiyo.
Mganga mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Singida (RMO) Bi. Doroth Bwajima akisoma taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Amesema baada ya mradi huo kukamilika mkoa wa Singida utaondokana na matatizo ya huduma za afya.
"Ili
kumuunga mkono Dk.Kone kwa hili jambo nzuri la ujenzi wa hospitali ya
rufaa ambayo itasaidia Watanzania wengi kupata huduma ya afya kwa
kiwango kizuri,nitahakikisha nina muunganisha na baadhi ya marafiki
zangu wa ndani na nje ya nchi ili waweze kusaidia kumalizika kwa ujenzi
wa hospaitali hii inayovutia",amesema Kinana.
Mganga
mfwawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, Dkt Joseph Malunda,
akiwaonesha michoro ya hospitali hiyo viongozi walioambatana na Kinana.
Viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakimsikiliza Dkt Malunda.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Pendael Maasai akisisitiza jambo kwa Kinana.
Muuguzi
Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Pendael Maasai
akimwonyesha Katibu Mkuu kinana vifaa mbalimbali vilivyopo kwenye
hospitali hiyo ya rufaa.
Mbunge MO akiangalia mojawapo ya vifaa vya hospitali ya rufaa ya singida.
Mbunge
wa Jimbo la Singida Mjini Mohammed Dewji akisalimiana na Daktari bingwa
wa magonjwa ya kina mama wa mkoa wa Singida Dkt, Seleman Mutani wakati
wa ukaguzi wa hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment