Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, January 20, 2015

BENKI YA NBC YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI SHULE YA MSINGI MAWENI-KIGAMBONI DAR ES SALAAM


 Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Hali Hatarishi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Nicholaus Paul (wa nne kushoto) akikata utepe kuashiria makabidhiano ya msaada wa madawati yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 3 yaliyotolewa na wafanyakazi wa kitengo cha mikopo ya makampuni cha benki hiyo kwa Shule ya Msingi Maweni. Hafla ya makabidhiano ilifanyika shuleni hapo, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Maweni, Sylvester Roche, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Martha Silavwe, Mwalimu Mkuu, Zuhura Mwaliko na baadhi ya wafanyakazi wa NBC.
 Meneja wa Kitengo cha Mikopo ya Makampuni wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC, Beatrice Musira (kulia) akisalimiana na mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Maweni, Msafiri Habakuki, wakati wa hafla hiyo shuleni hapo jana.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Maweni, Zuhura Mwaliko (katikati) akimshukuru  Mkuu wa Idara ya Mikopo Mikubwa ya Makampuni wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Salehe Mohamedi, baada ya kupokea msaada huo. Kulia ni Mkuu wa Usaidizi wa Biashara na Ukusanyaji wa Mikopo wa NBC, Faith Majiwa.
 Mmoja wa wafanyakazi wa enki ya NBC, Noela Ishebabi (kulia) akiwapa viburudisho wanafunzi wa shule hiyo wakati wa hafla ya makabidhiano ya madawati shuleni hapo jana.
 Baadhi ya wanafunzi waShule ya Msingi Maweni wakiimba kwa furaha wakati wakipokea msaada wa madawati kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), shulenihapo, Kigamboni, Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakipozi kwa picha na mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kuwasili shuleni hapo, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...