Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, January 9, 2015

MABONDIA IDDI BONGE NA ALIPHONCE MCHUMIATUMBO KUZIPIGA FEB 14


NA MWANDISHI WETU

MABONDIA wenye uzito wa juu nchini Aliphonce Mchumiatumbo na Iddi Kipandu 'Iddi Bonge' watapambana Feb 14 katika ukumbi wa P.T.A sabasaba wakigombania ubingwa wa taifa pamoja na pikipiki akizungumzia mpambano huo promota Shabani Manyoka amesema kupitia kampuni ya Mahamba Incorporation Limited wameamua kuandaa mpambano huo wa uzito wa juu ambao ni admu sana nchini kufanyika na ndio mabondia wanaokubalika Duniani kote

mpambano huo wa raundi kumi utakuwa ni wa aina yake kwa kuwa kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo bondia Iddi Mnyeke atapambana na Yonas Sego wakati Sahani Kaoneka atamkabili Saidi Mbelwa, na Deo Samweli akipambana na Adam Ngange Juma fundi atakabiliana na Bakari Ostadhi na Amani Bariki 'Manny Chuga' atapambana na Mohamed Kashinde siku hiyo pia kutakuwa na mpambano mwingine wa utangulizi wa uzito wa juu kati ya Bank Mwakalebela atakae mkabili Frank Kimbwilo

Manyoka aliongeza kwa kusema kuwa siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha ndani na nje ya ukumbi huo ambapo amesha wasiliana na walinzi mbalimbali
siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali 
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

2 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...