Wachezaji
wa timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars ‘ wakiwasili jana
katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam wakitokea nchini Uganda kushiriki michuano ya Cecafa Challenge
iliyomalizika juzi. Kilimanjaro Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro
Premium Lager.
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara
‘Kilimanjaro Stars ‘ wakiwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kuwasili wakitokea nchini Uganda
kushiriki michuano ya Cecafa Challenge iliyomalizika juzi. Kilimanjaro Stars
inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager. (Picha na Mpigapicha
wetu).
Kocha
Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Stars’ Kim Poulsen
akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuwasili katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana
pamoja na timu wakitokea nchini Uganda kushiriki michuano ya Cecafa
Challenge iliyomalizika juzi.
Na Mwandhishi Wetu
Timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars iliyoshiriki katika mashindano
ya Cecafa Challenge yaliyomalizika Jijini Kampala Jumamosi, imerejea
Jijini Dar es Salaam huku sasa ikitizamia kukutana na Chipolopolo ya
Zamzbia Disemba 23.
Stars, ambayo inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, ilirejea jana jioni kwa ndege ya Precision Air.
Kikosi hicho chenye wachezaji 18, kilifanikiwa kutinga nafasi ya nne
katika mashindano hayo baada ya kufungwa za Zanzibar Heros kwa penalty
6-5 na kutinga nafasi ya tatu.
Katika mashindano hayo, The Cranes ya Uganda ilifanikiwa kutetea taji na
kubakiza kombe nyumbani. Hii nimara ya 13 kwa Uganda kutwaa taji hilo.
Akizungumza baada ya kurejea, Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim
Poulsen alisema mashindano haya yalikuwa muhimu sana kwa timu yake kwani
vijana wamepata uzoefu baada ya kukutana na timu ngumu na zenye uzoefu.
“Mashindano yalikuwa mazuri…tulienda na nia ya kurudi na kombe lakini
hatujafanya jivyo ila muhimu ni kwamba mashindano haya yametupa uzoefu
mkubwa ili tuweze kujiandaa na mashindano mengine ambayo yako mbele
yetu,” alisema.
“Tumefarajika kucheza na timu kubwa kama The Cranes ambayo ndio timu
bora katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati,” alisema.
Alisema sasa hivi macho ya wachezaji yote yako katika mchezo ujao wa
kirafiki dhidi ya Chipolopolo ya Zambia kwani ni mechi ambayo itakuwa
kipimo kikubwa kwa Stars kwa hivyo inahitaji maandalizi makubwa sana.
“Nawaomba watanzania wasikate tama kwa kuwa tunaijenga timu hawa ni
vijana na ninaamini siku zijazo watafanya vizuri zaidi,” alisema
Poulsen.
Kocha Kim Poulsen anatarajiwa kutangaza kikosi cha Stars kesho Jumatatu
na amesema atawaita wachezaji wa Zanzibar pia ambao walicheza vizuri
Kampala.
“Niliwaona wakicheza kwa hivyo bila shaka waliofanya vizuri watakuwemo kwenye kikosi hiki,” alisema.
No comments:
Post a Comment