Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra Tanazania Asa Mwaipopo (wapili kushoto) akibadirishana nyaraka za makubaliano na Mkuu wa Kituo chaUshonaji cha Utete Tailoring Mart kilichopo Songea, Mkoani Ruvuma Atnas Nyumbi (katikati) wakati wa hafla ya kukabidhi cherehani ya kisasa itakayotumika kutengeneza sare za wafanyakazi wa Kampuni ya Mantra .Picha na mpiga picha wetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra Tanazania Asa Mwaipopo
(kushoto) akikabidhi cherahani ya kisasa kwa Mkuu wa Kituo chaUshonaji
cha Utete Tailoring Mart Atnas Nyumbi (kulia)ambayo itasaidia
kutengeneza sare za wafanyakazi wa Kampuni ya Mantra .Picha na mpiga
picha wetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra Tanazania Asa Mwaipopo (wapili
kushoto) akionyesha sare za wafanyakazi wa kampuni hiyo
zinazotengenezwa na Kituo chaUshonaji cha Utete Tailoring Mart kilicopo
Songea Mkoani Ruvuma wakati wa hafla fupi ya kukabidhi cherahani ya
kisasa kwa Mkuu wa Kituo hicho Atnas Nyumbi (kushoto)mwishoni mwa
wiki.Picha na mpiga picha wetu
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra Tanazania Asa Mwaipopo
(kushoto) na Mkuu wa Kituo chaUshonaji cha Utete Tailoring Mart
kilichopo Songe, Mkoani Ruvuma Atnas Nyumbi (kulia) wakitia sahihi hati
za makubaliano zitakazowezesha kituo hicho kutengeneza sare za
wafanyakazi wa Kampuni ya Mantra .Picha na mpiga picha wetu.
Na mwandishi wetu , Songea
KAMPUNI ya
Mantra Tanzania imeendeleza jitihada zake za kusaidia jamii
inayoizunguka kwa kutoa cherehani yakisasa inayotumia mfumo wa komputa
kwa Kituo cha Ushonaji cha Utete Tailoring Mart kilichopo mjini Songea ,
Mkoani Ruvuma.
Akizungumza
katika hafla fupi ya kukabidhi cherehani hiyo mwishoni mwa wiki,
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra Tanzania Asa Mwaipopo alisema
kuwa kampuni yake imejizatiti kusaida kupunguza umasikini kwa kusaidia
miradi mabali mbali ya maendeleo kwenye Mkoa huo wa Ruvuma.
Mwaipopo
alisema tayari kampuni yake imesaini hati za makubaliano na Kituo cha
Ushonaji cha Utete ambapo kituo hicho kitatengeneza sare (uniform) za
wafanyakazi wa kampuni yake hali ambayo itasaidia kujenga uwezo wa kituo
hicho.
“Kampuni ya
Mantra ina nia ya kusaidia miradi mbali mbali ya maendeleo kwakutambuma
umhimu wa miradi hiyo katika kupunguza umasikini. Kwa lengo hilo, leo
tunakabidhi cherehani ya kisasa kwa kituo hichi cha Utete na tunaamini
jitihada zetu zitakuwa chachu ya maendeleo ya kituo hiki.
Mwaipopo
alisema cherehani hiyo imetolewa kwa mtindo wa mkopo wa mzunguko
(Revolving Fund) na kusema kuwa pesa itakayopatikana itasaidia
kuendeleza washonaji wengine mkoani humo.
“Atalipia kwa
utaratiu wa kazi ambazo tutakuwa tukimpa kwa makato ya taratibu. Pesa
ambayo itapatikana itasaidia kuinua washoinaji wengine. Ni matumaini
yangu kuwa cherehani hii itatumika kwa matumizi sahihi iliiweze kuka
muda mrefu ,” alisema Mwaipopo.
Maipopo
alisema kuwa kampuni yake inatakribani wafanyakazi 150 na kusema kuwa
idadai hiyo itaongozeka maradufu kufikia wafanyakazi 1500 kipindi Mradi
wake wa Urani wa Mto Mkuju utakapoanza.
“Ni matumaini
yetu kuwa sare za wafanyakazi wote hao zitatengenezwa na kituo hich cha
Utete. Hii sikazi wa mtu mmoja kwahiyo lazima kituo hiki kiaajiri
washonaji wengine. Ni matumaini yetu kuwa wananch watachangamkia fursa
zitakazopatikana,” alisema.
Naye Mkuu wa
Kituo hicho cha ushonaji cha Utete Atnas Nyumbi alisema msaada huo
umekuja muda muafaka na kuahidi kutumia cherehani hiyo vizuri ilikupata
mafanikio makubwa zaidi.
“Tunashukuru
Kampuni ya Mantra kwa kuwa na imani na kituo chetu. Tunaahidi kutumia
cherehani hii vizuri ilituweze kupata mafanikio na kusonga mbele,”
alisema Nyumbi.
Kampuni ya
Mantra Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kusadia miradi mbali
mbali ya maendeleo kwenye Mkoa wa Ruvuma ikwemo miradi ya afya, elimu,
utunzaji wa mazingira pamoja na michezo.
No comments:
Post a Comment