CHAMA cha Wananchi (CUF) Wilaya ya
Handeni, kimekiri kumiliki migodi ya madini minane mkoani Tanga huku kikiwataka wananchi kupuuza
tuhuma zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa kuwa hawamiliki kihalali migodi
hiyo.
Akihutubia kwenye mkutano wahadhara
Katibu wa CUF Wilaya ya Handeni Masoud Mjaila alisema Chama hicho kina Kampuni
halali inayomiliki migodi hiyo minane ya madini mbalimbali kwenye Kijiji cha
Sezakofi kata ya Ndolwa.
Huku akionyesha baadhi ya nyaraka za
kampuni yao inayomiliki migodi hiyo Mjaila, aliwaonya wakazi wa handeni kuwa
macho na wanasiasa wanaohama hama kwenye vyama na kuanzisha vyama vipya kuwa ni
watu hatari na wakuogopwa.
Chama hicho kililazimika kutoa maelezo
hayo mbele ya wananchi kufuatia tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na Chama
kipya Cha Kisiasa Cha ADC kupitia mlezi wa Chama hicho Doyo Hassan Doyo
aliyedai kuwa chama hicho kina miliki migodi bila ya kuwa na vibali.
“Wananchi msikubali kuburuzwa, hiki
chama chenu cha CUF kina miaka 20 tangu kuanzishwa, hapa Handeni kina miaka 15,
lakini mnaona hali ilivyo, ndiyo hivi karibuni sasa na sisi tupo ndani ya
Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema Mjaila na kuongeza:
“Sasa hawa ADC wameanza jana, leo
wanataka waungwe mkono, hapana! Hawa wanatafuta masilahi yao maana huku CUF
walifukuzwa.
“Eti wanasema migodi ile ya madini haina
vibali, siyo kweli kwani serikali iko wapi, tumechangia zaidi ya Sh3.5 milioni,
kusaidia miradi mbalimbali ya Serikali ya Kijiji cha Sezakofi.”
Hata hivyo Chama hicho kilitoa vitu
mbalimbali kwa Hospitali ya Wilaya hiyo vikiwemo mashuka yenye thamani ya Tsh120,000 na sabuni zenye
thamani ya Tsh 150,000.
Mjaila aliwataka wanasiasa kutumia fursa
zilizopo kuleta maendeleo nchini kuliko kuendeleza siasa za kupakana matope
majukwaani haziwasaidii wananchi
No comments:
Post a Comment