Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, January 16, 2013

MALINZI, NYAMLANI WATAKA URAIS TFF


Mgombea wa nafasi ya Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF. Othumani Nyamlani  (kulia) akichukua fomu ya kugombea nafasi hiyo Dar es salaam jana kwa mmoja wa maofisa wa TFF. Jonathan Kakwaya Dar es salaam leo mwingine ni Mwenyekiti wa chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya, Elias Mwanjara.Picha na www.burudan.blogspot.com
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF.Jamal Malinzi  (kulia) akiludisha fomu ya kugombea nafasi hiyo Dar es salaam leo kwa mmoja wa maofisa wa TFF. Jonathan Kakwaya. Dar es salaam jana.Picha na www.burudan.blogspot.com
HARAKATI za kuwania urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) sasa zimeanza kushika kasi baada ya wanamichezo wawili maarufu nchini kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo. Wanamichezo hao, Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani na Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Kagera, Jamal Malinzi walichukua fomu hizo jana. Mgombea mwingine aliyechukua fomu jana kwa ajili ya kuwania nafasi hiyo ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Kigoma, Omari Mussa Nkwarulo. Malinzi alichukua fomu ya kuwania nafasi hiyo kwa njia ya mtandao na kuirejesha jana, akiwa ameambatanisha ada ya sh. 500,000 wakati Nyamlani alichukua fomu hiyo katika ofisi za TFF na kuijaza papo hapo kabla ya kuirejesha. Malinzi aliwahi kuwa katibu mkuu wa klabu ya Yanga mwishoni mwa miaka ya 1990 na pia aliwahi kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi wa mwaka 2008, lakini alipigwa mweleka na rais wa sasa wa TFF, Leodegar Tenga. Kwa upande wake, Nyamlani amewahi kuwa katibu wa Chama cha Soka wilaya ya Temeka (TEFA) na pia katibu wa Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA). Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema jana kuwa, hadi sasa jumla ya wagombea 30 wamechukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa shirikisho hilo. Akizungumza baada ya kurejesha fomu yake, Malinzi alisema anampongeza Tenga kwa kufanya maamuzi magumu ya kutogombea tena nafasi hiyo. Malinzi alisema hali hiyo inawafanya wapiga kura watakaoshiriki katika uchaguzi huo kufanya maamuzi sahihi kwa kumchagua kushika nafasi hiyo kwa vile ana uwezo wa kuliongoza shirikisho hilo. "Naaamini kuwa wapiga kura watakuwa na imani na mimi kwani si mara yangu ya kwanza kuomba nafasi hii, niliomba mwaka 2008, lakini kura hazikutosha," alisema Malinzi. Naye Nyamlani alisema ameamua kuwania nafasi hiyo kwa lengo la kuendeleza soka ya Tanzania, kazi iliyokuwa ikisimamiwa vyema na Tenga, ambaye yeye ni msaidizi wake mkuu. "Nadhani mimi ndiye ninayefaa kuendeleza kazi hiyo na iwapo nitachaguliwa, nitaifanyakazi hiyo kwa umakini mkubwa na kutilia mkazo programu ya kuendeleza soka ya vijana,"alisema Nyamlani, ambaye alisindikizwa na kundi kubwa la wapambe Mgombea mwingine aliyechukua fomu jana ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Elias Mwanjala anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuwakilisha Kanda ya Iringa na Mbeya. Orodha kamili ya wagombea waliochukua fomu ni Athumani Nyamlani, Jamal Malinzi na Omari Nkwarulo (urais), Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (umakamu wa rais). Wanaowania ujumbe wa Kamati ya utendaji, kanda zao katika mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza), Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly Mbise (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa). Wengine ni James Mhagama (Njombe na Ruvuma), Athuman Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es Salaam).

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...