JOHANNESBURG, Afrika Kusini
“Soka lililooneshwa na Cape Verde katika kuwania kufuzu AFCON 2013, halitoi nafasi kwa nyota wa Bafana kujivunia uenyeji, bali upiganaji wa kweli na kutambua ukubwa wa jukumu walilonalo. Wajifunze kwa Cameroon, ambao waliteswa na Cape Verde”
WENYEJI wa fainali za Kombe la Mataifa Afrika 2013, timu ya
taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’, leo wanajitupa kwenye Uwanja wa Taifa
‘Soccer City’ jijini hapa, katika mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo dhidi ya
timu ya taifa ya Cape Verde.
Pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa
Bafana Bafana, litachezwa saa 12 kwa saa za hapa, huku wachambuzi wa soka barani
Afrika wakitaka kujua kile kinachoweza kufanywa na wenyeji hao chini ya kocha
Gordon Igesund.
Wachambuzi hao hawataraji mteremko kwa Bafana Bafana katika
mechi hiyo, kutokana na soka lililooneshwa na Cape Verde chini ya kocha Lucio
Antunes katika michuano ya kuwania kufuzu fainali hizi, ilikopangwa kundi moja
na Cameroon iliyoshindwa kufuzu.
Kocha wa Bafana, Igesund amewataka nyota wa kikosi chake
kutojivunia uenyeji, badala yake kupiganmia heshima ya kuanza vema na kujenga
imani mongoni mwao na mashabiki wanaoawaunga mkono.
“Soka lililooneshwa na Cape Verde katika kuwania kufuzu
AFCON 2013, halitoi nafasi kwa nyota wangu kujivunia uenyeji, bali upiganaji wa
kweli na kutambua ukubwa wa jukumu lao. Wajifunze kutoka kwa Cameroon, ambao
waliteswa na Cape Verde,” alisema Igesund.
Baada ya kumalizika kwa pambano hilo, mashabiki watapata
fursa ya kushuhudia webnyeji wa fainali za mwaka 2010, timu ya taifa ya Angola
wakishuka kwenye uwanja huo huo kukipiga na Morocco.
Angola inayonolewa na Gustavo Ferrini na Morocco chini ya
kocha Rachid Taoussi, zitaumana dimbani hapo kuanzia saa 3:00 usiku kwa saa za
hapa, katika pambano jingine la kuvutia – linalohusisha timu ya kusini mwa
Afrika.
No comments:
Post a Comment