Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa
Tanzania, kupitia Baraza la Sanaa la Taifa, limebariki kufanyika kwa
Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13 baada ya kuridhishwa na
maandalizi yaliyo fanywa na Miss Tourism Tanzania Organisation
waandaaji wenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha mashindano hayo
kitaifa na kimataifa, pia kwa kuzingatia sheria za nchi, kanuni na
Taratibu za mashindano.
Serikali pia imeridhishwa na jinsi
Fainali za ngazi za mikoa na kanda zilivyofanyika kwa mafanikio,ambapo
kila mkoa umepata washindi wenye sifa za kuwakilisha mkoa husika katika
Fainali za Taifa mwaka huu,ambapo jumla ya warembo 60 waingia rasmi
kambini kesho katika hoteli ya Ikondelelo Lodge Dar es Salaam, kuanza
mbio za kuwania Taji
hilo la Taifa.
Washindi wa 1-5 wa Fainali za Taifa
,watawakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya Dunia yakiwemo
ya International Miss Tourism World, Miss Tourism United Nation, Miss
Heritage World, Miss Tourism University World, Miss Globe International
n.k
Miss Utalii Tanzania ,hadi sasa
tunashikilia Jumla ya mataji 5 ya Dunia na kimataifa, yakiwemo ya Miss
Tourism World 2005-Africa,Miss Tourism World 2006-SADC,Miss Tourism
World 2007-Africa, Miss Tourism Model Of The World 2008-Personality n.k
Fainali za Taifa mwaka huu zimepangwa
kufanyika wiki ya kwanza ya Februari ,wilaya ya Temeke na mkoa wa Dar
es Salaam ukiwa umepewa heshima ya kuwa wenyeji wa Fainali hizo.
Asante,
Erasto Gideon Chipungahelo
Rais
No comments:
Post a Comment