Na
Elizabeth John
RAIS wa IBF katika bara la Afrika,
Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Mtanzania Onesmo Ngowi anatarajia kuwa
msimamizi Mkuu katika pambano la ubingwa wa dunia la vijana katika jiji la
Johannesburg nchini Afrika ya Kusini.
Ngowi anatarajiwa kuwa msimamizi
Mkuu katika mpambano huo utakaowakutanisha mabondia Ilunga Makaba kutoka
Jamhuri ya Kidokrasia ya Kongo (DRC) mwenye makazi yake nchini Afrika ya Kusini
na Gogita Gorgiladze anayetoka katika jiji la Tiblis, nchini Georgia.
Ngowi alisema, pambano la wawili hao
wenye wiwango vinavyolingana Georgita (12) na Makaba (12) watapambana kugombea
mkanda wa vijana wa wa dunia (Youth Title) wa Shirikisho la Ngumi la Ngumi la Kimataifa
(IBF) katika uzito wa Cruiserweight Februari 15 mwaka huu katika hoteli ya
nyota 5 ya Emperors Palace in Kempton Park, Gauteng katika jiji la
Johannesburg.
Ngowi kama kamishena mkuu wa pambano
hilo atasaidiwa na maofisa wafuatao ambapo mwamuzi ni Wally Snowball, Jaji
namba moja Simon Xamlashe na namba tatu Jaap Van Niewenhuizen wote kutoka
(Afrika Kusini) pamoja na Jaji namba
mbili Manuel Maritxalar (Spain).
Aliongeza kuwa pambano hilo ni kati
ya mapambano zaidi ya 100 ya IBF yatakayofanyika katika bara la Afrika, Ghuba
ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika kipindi cha mwaka huu wa 2013 chini ya uradi
wa IBF
No comments:
Post a Comment