Na
Elizabeth John
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Emmanuel Elibariki
‘Nay wa Mitego’ amesema wimbo wake wa ‘Nasema Nao’, ambao unafanya vizuri
katika vituo mbalimbali vya redio na runinga, ni hisia zake binafsi na wala
hana bifu na mtu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo,
Nay, alisema kuwa alifanikiwa kurekodi wimbo huo baada ya kufika studio na
kukuta mapigo bila wimbo, na ndipo alipoamua kufanyia mazoezi kabla ya
kuirekodi na kuisambaza.
Nay, alisema hakukusudia kumsema mtu, licha ya baadhi ya
maneno ya wimbo huo kuwa na majina ya wasanii na viongozi, lakini lengo lake ni
kufikisha ujumbe kwa jamii na si vinginevyo.
“Mimi ndiye msanii wa kwanza wa muziki wa kizazi kipya
kutaja watu kwenye nyimbo nikiwa na lengo la kufikisha ujumbe ninaoukusudia kwa
jamii, na humu simaanishi chochote kibaya,” alisema Nay Wa Mitego.
Mkali huyo wa Bongo Fleva, alisema katika hilo, hana ‘bifu’
na mtu yeyote na hatarajii kusikia akiingia katika malumbano na wasanii
waliotajwa katika wimbo huo ambao unafanya vizuri katika redio mbalimbali
nchini.
No comments:
Post a Comment