Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na Mkuu wa
Wilaya ya Kyerwa, Darry Rwegasira katika Hifadhi ya Rabanda-Rumanyika,
alipoitembelea kuona shughuli za uhifadhi na kudhibiti ujangili nchini.
(Picha zote na Mpiga Picha Wetu)
Naibu
waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiangalia nyaya
mbalimbali zilizokamatwa kutoka kwa majangili wanaovamia hifadhi za
Burigi na Biharamulo Rumanyika alipotembelea ili kuona shughuli za
uhifadhi na kudhibiti ujangili nchini.
DAR ES SALAAM, Tanzania
SERIKALI
imeshangazwa na hatua ya wageni kuwavamia mbuga mbalimbali na misitu
nchini kiasi cha kufanya kuongezeka vitendo vya ujangili na kuahidi
kuchukua hatua kali ili kutokomeza ujangili huo.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema ili kudhibiti
hali hiyio hatua za haraka zinahitajika kuchukuliwa ikiwamo na
kuimarisha ulinzi katika hifadhi na mapori mbalimbali ambayo mengine
yameanza ktumiwa na waasi.
Akizungumza
mjini Bariadi baada ya kuwaona askari wa Kijereshi walioko mahabusu kwa
kutuhumiwa kuua majangili, Nyalandu alisema kuwa askari wakliopo ni
wachache kiasi cha kufanya majangili wengi kuvamia hifadhi na kuua
wanyama hususan tembo.
“Kinachosikitisha
ni kuwa hawa majangili wamebadilika zamani waklikuwa wanawinda kwa
ajili ya kupata kitoweo lakini sasa wamebadilika na wanavamia kwa silaha
za kijeshi na kuua wanyama bila woga” alisema.
Nyalandu
aliahidi kuwa kwa sasa hali hiyo imekuwa kama janaga la kitaifa na
hivyo kutaka wananchi kubadilika na kkabiliana na majangili ili kulinda
maliasili kwa ajili ya vizazi vijavyo.
“Tnahitaji
kuajili vijana wengi kadri inavyowezekana ili kukabiliana na wimbi
hili, tunahitaji zaidi ya askari 4,000 na kuanzia mwaka huu tumepewa
kibakli cha kuajili vijana 400 ambao tutawasambaza katiak hifadhi na
mbuga nyingine.
Alisisitiza
kuwa kwa sasa askari hao wanalinda zaidi ya kilometa za maraba 169
wakati zinazotakiwa ni kilometa za mraba 25 na hivyo kutoa mwanya kwa
majangili kuingina na kutoka bila ya kupatikana.
Nyalandu
alisema nchi ilitalajiwa kuwa na tembo 400,000 mwaka huu miaka 50
iliyopita na kini kutokana na kukithiri vitendo vya ujangili wamebakia
tembo 110,000 tu kitu kinachotishia uwepo wa wanyama hao.
No comments:
Post a Comment