Mjasiriamali
Elizabeth Chami (26), akioka keki kwenye jiko la kisasa alilozawadiwa
na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia promosheni ya Safari Lager
Wezeshwa 2012, kwenye karakana yake iliyopo Tabata Mawenzi, Dar es
Salaam.
Mfanyakazi wa karakana hiyo, Happiness akiandaa keki kwenye jiko hilo la kisasa.
Mfanyakazi
wa Kiwanda cha kutangeneza Shampoo cha L &, V Intergrated Firm,
kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam, Hashim Hussein, akipaki katoni za
bidhaa hiyo. Kiwanda hicho kilisaidiwa chupa 15,000 baada ya mmiliki wa
kiwanda hicho Valerian Luzangi (hayupo pichani) kuwa mmoja wa washindi
wa promosheni ya Safari Lager Wezeshwa 2012.
Luzangi, akisaidia kupanga vizuri chupa zilizojazwa shampoo. Kushoto ni mfanyakazi wa kiwanda hicho Stahabu Mwinyi.
Mjasiriamali
Valerian Luzangi (38), kulia, akipanga vizuri katoni za shampoo
anazozalisha katika kiwanda chake cha L & V Intergrated Firm,
kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam juzi. Luzangi alisaidiwa chupa 15,000
baada ya kuwa mmoja wa washindi wa promosheni ya Safari Lager Wezeshwa
2012, Kushoto ni mfanyakazi wake, Hashim Hussein.
Wajasiriamali
Innocent Mberwa (kulia) na Gosbert Mugisha, wakiweka sawa mfumo wa
umwagiliaji katika moja ya mashamba ya zao la matikiti maji ya Kampuni
yao ya Tin Wax eneo la Minondo, Kata ya Somangila, Kigamboni, Dar es
Salaam juzi. Kampuni hiyo ilizawadiwa mfumo huo baada ya kushinda
promosheni ya Safari Lager Wezeshwa 2012.
Mjasiriamali
Innocent Mberwa akionesha tikiti maji katika moja ya mashamba ya
Kampuni yao ya Tin Wax yaliyopo eneo la Minondo, Kata ya Somangila,
Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kampuni hiyo ilizawadiwa mfumo wa maji wa
umwagiliaji baada ya kushinda promosheni ya Safari Lager Wezeshwa
2012,
Baadhi ya vitunguu vinavyozalishwa katika shamba hilo. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO.
No comments:
Post a Comment