Wakati kesho
ndiyo mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu za kuwania uongozi kwenye
uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi
Kuu Tanzania (TPL Board) waombaji 36 wameshachukua na 18 tayari
wamesharejesha.
Idadi hiyo ni
kufikia leo mchana (Januari 17 mwaka huu). Pia Kamati ya Uchaguzi ya TFF
inasisitiza kuwa wanaorejesha fomu hizo kwa email wanatakiwa kuzituma
kwa Katibu Mkuu wa TFF kwa email ya tfftz@yahoo.comna si kwa email binafsi za wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi au maofisa wa TFF.
Waombaji wanne
walioongezeka katika orodha ni Blassy Kiondo kwa Kanda ya Katavi na
Rukwa, Eliud Mvella (Mbeya na Iringa), Geofrey Nyange (Morogoro na
Pwani), na Omari Abdulkadir kwa Kanda ya Dar es Salaam.
Orodha kamili
ya waombaji ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo
(urais) wakati waombaji wa umakamu wa rais mpaka sasa ni Michael
Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia.
Kwa upande wa
wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama
(Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na
Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra Swai
na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly Mbise
(Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo,
Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa)
na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).
Athuman Kambi
na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima
(Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Geofrey Nyange na Twahili Njoki
(Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala na Eliud Mvella (Iringa na Mbeya),
Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Omari
Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).
Kwa upande wa
Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) waliochukua fomu mpaka sasa ni wawili tu.
Yusuf Manji amechukua fomu ya uenyekiti wakati Said Mohamed amechukua
fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti.
SUPER WEEK TENA NDANI YA LIGI KUU YA VODACOM
Mzunguko wa
pili ya Ligi Kuu ya Vodacom utaanza Januari 26 mwaka huu huku kukiwa na
maombi ya televisheni ya SuperSport kuonesha mechi za Super Week kama
ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza.
Raundi tano za
awali katika ratiba ya mzunguko wa pili zinabaki kama zilivyo wakati
nyingine zilizobaki zitatolewa baada ya kuingiza mechi za Super Week.
Wakati
huo huo, mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza unatarajia kuanza
Januari 26 mwaka huu. Ratiba ya ligi hiyo na tarehe rasmi ya kuanza
itatangazwa baada ya kupitiwa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) inayotarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment