Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi akifafanua jambo wakati wa kuchezesha droo hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi (katikati) akimsikiliza kwa
makini Meneja wa benki hiyo tawi la Kariakoo, Maduhu Bulebi Makoye
wakati wa kuchezesha droo hiyo. Kushoto ni Meneja Mkuu Mauzo na Huduma
kwa Wateja, Grace Nkuzi.
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Posta Tanzania (TPB), imetangaza
washindi watatu wa promosheni ya Shindano la kutumia huduma ya Weastern
Union, ambalo ni la pili, baada ya lile la mwaka jana.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi amesema kuwa washindi hao watatu
wamepatikana baada ya droo iliyochezeshwa mbele ya waandishi wa habari.
"Washindi hao wametoka katika
matawi mbalimbali ya Benki ya Posta nchini ambapo zawadi ya kwanza na ya pili
zimebaki jijini Dar es Salaam na ile ya tatu kwenda mkoani Arusha".
Moshingi aliwataja washindi hao kuwa ni
pamoja na James Mkondya aliyejinyakulia sh milioni mbili, Ensel Issa, sh
milioni mojawote hao wakazi wa jijini na Kaeni Kapangi aliyejinyakulia sh
700,000 mkazi wa Arusha.
Aidha,
washindi wengine kumi wamejipatia
zawadi ya sh 100,000 kila mmoja.
Moshingi alitoa wito kwa Watanzania kujiunga
na huduma za Benki hiyo kwani zimboreshwa na kuwafanya wateja wake kwenda na
wakati katika shughuli zao zakujiletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment