DAR ES SALAA, Tanzania
Naye
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (DP), Christopher Mtikila, amemtaka Rais
Kikwete kutumia hekima katika kumaliza mgogoro wa gesi na maslahi ya Mtwara
kinyume chake nchi inaweza kugawanyika.
Akizungumza
na wandishi wa habari Dar es Salaam leo, Mtikila alisema kuwa madai ya kwamba
umeme wa gesi hiyo ufuliwe kulekule Kusini yanatokana na uchungu wa wananchi
wote wa Kusini.
Alisema
iwapo moto wa mgogoro huo hatauzimwa kwa hekima si ajabu ukaimeza mikoa yote ya
Kusini ikiwemo Lindi, Ruvuma, Mbeya, Iringa,
Morogoro na hata Rukwa ambapo matokeo
yake kuzaliwa mataifa mawili mpaka ukiwa reli ya kati.
Mtikila
alisema wakazi wa kusini hawazuii gesi hiyo isitoke bali wanachotaka umeme huo
ufuliwe kule kule, lengo likiwa ni kuwaletea mapinduzi ya maendeleo.
“Wananchi
wa Mtwara wanafahamu kwamba sumaku ya mandeleo ya uwekezaji wa miradi mikubwa
ya kuwaletea maendeleo ni nishati na miundombinu, lakini watawala wa CCM
waliwanyang’anya reli ya kusini kwa uharamia wa kung’oa mpaka mataruma na kufutilia
mbali hata na tuta lenyewe,”alisema.
Aliongeza
kuwa Rais Kikwete analazimika pia kutamka bayana kipaumbele kwa uboreshaji wa
Bandari Kuu ya Mwara, ikibidi hata kwa kusitisha mradi wa Bandari ya Bagamoyo.
Kwamba
njia pkee ya kuzima moto huo kusini na kurejesha amani ni Rais huyo kutoa tamko la kukubali kufuliwa
umeme huo mkoani Mtwara kwa ajili ya maslahi ya Taifa.
No comments:
Post a Comment