Msanii Lulu (katikati) akisubiri kusikiliza maombiyake ya dhamana kusomwa na Jaji anaesikiliza kesi hiyo Zainabu Mruke leo jijini Dar es Salaam. |
Lulu akiwasili kwenye kizimba cha Mahakama kuu jijini Dar es Salaam leo. |
Kama ilivyo sikuzote ulinzi uliimarishwa kwenye mahakama hiyo wakiwemo askari wakiume pamoja na wakike kumlinda msanii huyo. |
Baada ya kusomewa mashart ya dhamana Lulu akiondoka huku akitokwa na machozi yanayoashiria furaha. |
Ndugu jamaa na marafiki wa msanii huyo na baadhi ya watu wengine wakiwa kwenye Chumba cha mahakama kuu jijini Dar es Salaam wakisubiri kusikiliza maombi ya dhamana. |
Msanii Muhusin Awadi (Dk.Cheni) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutolewa kwa dhamana ya msanii huyo. |
Wakili wa Lulu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mteja wake kupatiwa dhamana. |
HATIMAYE
Msanii wa Filamu nchini Elizabeth Michael maarufu
kwa jina la Lulu mchana wa leo amepata dhamana na kuachiliwa kutokana na kesi
inayo mkabili ya kuua bila kukusudia msanii mwenzake wa filamu marehemu Steven
Kanumba mwaka jana.
Akisoma mashart ya dhamana Jaji
anaesikiliza Kesi hiyo Zainabu Mruke, alitaja mashart kadhaa ambayo mtuhumiwa
atatakiwa kuyatekeleza kabla ya kupewa dhamana hiyo.
Mruke alisema mtuhumiwa atatakiwa
kuwasilisha hatizake za kusafiria zote mahakamani hapo, atatakiwa kuwa na wadhamini
wawili wafanyakazi wa serikali ambao kila mmoja atatakiwa kuweka udhamini wa
Tsh20Millioni kama bondi na sio keshi.
Aidha Jaji Mruke aliongeza kuwa mtuhumiwa
hataruhusiwa kusafiri nnje ya jiji la Dar es Salaam isipokuwa kwa ruhusa maalum
ya mahakama, lakini pia atatakiwa kuripoti mahakamani kilatarehe moja ya kila mwezi.
Wakili wa mshtakiwa huyo Peter Kibatala
alisema amefurahishwa na dhamana aliyopatiwa mtejawake na wataendelea na kazi
ya kumtetea hadi mwisho wa kesi hiyo.
Wasanii wenzake waliojitokeza na kuonekana
mahakamani hapo ni pamoja na Muhusin Awadh (Dk.Cheni) na Steve Nyerere.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hukumu hiyo Dk.Cheni alisema
yeye binafsi amefurahishwa na dhamana hiyo na yuko tayari kufanyanae kazi.
“Lulu nilimchukua kwao akiwa na miaka mine
na kuanza kufanyanae kazi hadi sasa akiwa na umri wa miaka 18 amekua msanii
mkubwa nan i Director mzuri pia kwahiyo nitaendelea kufanyanae kazi”Alisema
Dk.Cheni.
Alipoulizwa kuhusu kutimiza Mashart ya
dhamana Dk.Cheni alisema kila kitu kilikuwa kimetimia ispokuwa passport tu ndio
hawakutarajia kama ingehitajika lakini tayari alishapigiwa simu mtu ailete
kutoka nyumbani kwao Tabata na kukamilisha mashart ya dhamana hiyo.
April saba mwakajana msanii
huyo alifikwa na kadhia hiyo ya tuhuma za kumuua bila kukusudia msanii
mwenzake wa Filamu nchini marehemu Steven Kanumba kutokana na mgogoro
uliotokana na wivu wa kimapenzi, baada ya kuelezwa kuwa wawili hao
walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.
zaidi tembelea http://www.saidpowa.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment