Baadhi ya wachezaji wa timu ya Black Leopards ya
Afrika Kusini wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam
jana. Timu hiyo inashuka dimbani leo kupambana na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa
katika mchezo wa kirafiki.
Kikosi cha timu ya Black Leopards kikiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili leo.
DAR ES SALAAM, Tanzania
WAKATI mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati, Yanga kesho watacheza mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini, kocha wa Black Leopards ametema cheche na kusema wataibuka na ushindi mkubwa kutokana na uzoefu wao wa mashindano ya Kimataifa.
Mchezo
huo umepangwa kuanza saa 10.00 jioni na maandalizi yake yamekwisha
kamilika huku waandaaji wakipunguza viingilio ili kuwawezesha mashabiki
wengi kufika.
Mratibu
wa mechi hiyo, Shafii Dauda wa Prime Time promotion alisema jana kuwa
maandalizi yote yamekamilika na wamepunguza kiingilio cha shs 5,000 na
shs 7,000 na kuwa cha shs 3,500 ili kuwafanya mashabiki wengi kuona
mechi hiyo.
Viingilio
vingine ni shs 7,000 kwa viti vya rangi ya machungwa, wakati VIP C ni
shs 15,000 , VIP B shs 20,000 na VIP A shs 30,000
Dauda
alisema kuwa Black Leopards wamewasili na kutamba kushinda mechi hiyo
kutokana na uzoefu waliopata katika mashindano mbali mbali ikiwa pamoja
na kombe la Shirikisho.
Kocha
wa timu hiyo, Abel Makhubela alisema kuwa wanauzoefu wa siku nyingi na
walifanya ziara nchi mbali mbali katika afrika na kuja Tanzania ni moja
ya faraja kwao.
“Ziara
hii ziara yetu ya kwanza Tanzania, tumefanya ziara nchini Zimbabwe na
nchi nyingie, tulipata matokeo mazuri na vile vile tunatarajia kupata
matokeo mazuri hapa, nimekuja na wachezaji wangu wote wa kikosa cha
kwanza, jumla ya wachezaji ni 23, mashabiki watarajie mchezo mzuri,”
alisema Makhubela.
Alisema
kuwa wanaijua Yanga na Simba ni moja ya timu nzuri na maarufu bara la
Afrika na hivyo wamejiandaa kwani ni kipimo kizuri cha ligi ya kwao
ambayo ipo katikati..
No comments:
Post a Comment