Mchungaji
wa Kanisa la EAGT la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi (57), Jana
alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Mkoa
wa Mbeya Gilbert Ndeuluwo akituhumiwa kumbaka na kumpa Mimba
mwanafunzi.
Akisoma
mashtaka hayo Mwendesha mashtaka wa Serilkali Archiles Mulisa alidai mshtakiwa
huyo alitenda kosa hilo kati ya Mwezi Januari 2008 ambapo alimbaka na kumpa
ujauzito Neema Boni (17) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari Itende.
Mulisa
alidai mahakamani hapo kuwa kosa hilo ni kinyume cha kanuni ya elimu ya 5 ya
gazeti la Serikali namba 265 ya mwaka 2003 na chini ya Sheria ya elimu namba 25
ya mwaka 1978 ambapo mshtakiwa anatuhumiwa kutenda makosa mawili ikiwemo kubaka
na kusababisha ujauzito.
Aliongeza
kuwa kosa la kubaka ni kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu cha 130(1),(2)(e)
na cha 131(1) kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Hata
hivyo mshtakiwa huyo alikana mashtaka yote ambapo aliachiwa kwa dhamana
ya Shilingi Milioni Mbili na mdhamini mmoja mwenye barua kutoka taasisi
inayotambulika, kesi hiyo iliahirishwa hadi Januari 30 itakapoanza kusikilizwa.
picha na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment