Na Bryceson Mathias, Vumila Kilindi
KAMPUNI
ya Udalali ya Jupitor Auction Mart ya Korogwe imetuhumiwa kutumia Jina
la Rais Jakaya Kikwete kuvunja nyumba ya Meleji Salunge (39) wa
Kitongoji cha Vumila, Kata ya Kinde Kilindi (W) na kuacha ya Juma
Nassoro, huku wakidaiwa kupora Mil. 100/- kwenye Godoro.
Malalamiko
hayo yalitolewa na Salunge kwa simu alipokuwa akitoka kituo cha Polisii
Songe ambako anadai hakupata Ushirikiano kama ilivyokosa kwa Mwenyekiti
wa Serikali ya Kijiji Juma Abdalahamani, ambapo sasa amehifadhiwa na
ambao hawakuvunjiwa.
Akizungumzia
tukio la Uvunjaji Salunge alisema, walifika watu watatu Ismail
Mwinchande, Kimanzi Msafari na Salum Sokoro toka Korogwe, ambapo alidai
wametumwa na Rais Jakaya Kikwete na ndipo walianza kufumua mabati ya
nyumba bila kuwapa Notisi na kutoweka na Mil.100/- zilizokuwa kwenye
Godoro.
“nilipofanyiwa
unyama , niliwaona viongozi wa Serikali ya Kijiji akiwemo Mwenyekiti wa
Serikali Abdalahamani nikakosa msaada, Diwani wa Kata ya Kinde Bonge
na Polisi Songe nao hawajanisaidia chochote nikarudi na kuhifadhiwa na
wasamaria vyombo vikiwa nje”,alisema.Salunge ambaye ni Mkulima.
Mwandishi
aliongea na Sokoro na kudai yeye si Msemaji isipokuwa Mkurugenzi Msafiri
au Kaimu Mwinchande, na kukanusha yeye na viongozi wake kupora Mil.
100/- akisema hao wanatapatapa kwani walipokwenda kuvunja nyumba hiyo
ambayo si ya waliyemkusudia, Sheria zilizingatiwa na walikwenda na
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Abdalahmani.
Kaimu
Mkurugenzi wa Jupitor Mwinchande alipohojiwa alisema, wao wamepewa
kibali na Baraza la Ardhi Korogwe, Madai ya kwamba wametumia Jina la
Kikwete kuvunja nyumba hiyo siyo ya kweli, ila mdaiwa Nassoro anawatumia
aliowauzia Ardhi ya ndugu yake aliyeko Negero Mvomero kinyemela, ili
kuichafua Kampuni, lakini akamtuhumu kutumia Morani wa kimasai
kuwatishia maisha.
Aidha
Mbunge wa Kilindi Beatrice Shelukindo alipotafutwa kwenye simu ili
kuzungumzia Sakata hilo simu yake haikupatikana, lakini Mkuu wa Wilaya
hiyo Selemani Livowa alisema yuko kwenye kikao atawasiliana na mwandishi
baadaye.
No comments:
Post a Comment