Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, March 29, 2013

300 WATHIBITISHA KUSHIRIKI SOKOINE MARATHON APRILI 12 MWAKA HUU


JUMLA ya wanariadha wapatao 300 wameshathibitisha kushiriki mbio za kumbukumbu za kifo cha hayati Waziri Mkuu na mpambanaji wa uhuru wa nchi hii, Edward Moringe Sokoine ambazo zinatarajiwa kufanyika Aprili 12 wilayani Monduli, Mkoani Arusha.
 
Wanariadha kutoka katika mikoa ya Kilimanjaro,  Manyara, Tanga, Dar es salaam na Arusha wameshathibitisha kushirki katika mbio hizo za kwanza kufanyika katika historia ya nchi hii tangu uhuru.

Hayo yamebainishwa na mratibu wa mbio hizo ambaye pia ndiye mwongozaji wa mbio hizo, Wilhelm Gidabuday akizungumza na LENZI YA MICHEZO  kwa njia ya simu kutoka ARUSHA na kusema kwamba tayari kupitia ofisi za chama cha Riadha mkoa Arusha (ARAA), wamethibitisha kushiriki mbio hizo.




Gidabuday alisema kuwa kujitokeza kwa wanariadha hao ni ishara nzuri kwani pamoja na kwamba ndio mara ya kwanza, kwa muitikio huo, wanatarajia kuwa na washiriki zaidi ya 500.

“Tumeshapata maombi kutoka kwa wanariadha kutoka katika mikoa mbalimbali tofauti na Arusha, kutokana na Taarifa ya ARAA, tayari kuna idadi ya wanariadha mia tatu, tunatarajia kuwa na wakimbiaji zaidi ya mia tano,” alisema Gidabuday.

Kuhusu zoezi la usajili, Gidabuday alisema kuwa zoezi hilo litaanza mapema baada ya sikuukuu za Pasaka kumalizika na kuongeza kuwa zoezi hilo litafanyikia katika Ofisi za ARAA, zilizoko katika uwanja wa mpira wa miguu wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kwa ada ya sh. 2000 za Tanzania.
 
Sokoine Marathon inatarajia kukukutanisha watu wa kada mbalimbali, wakiwemo viongozi, wabunge, mawaziri na wananchi kwa ujumla kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Hayati Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine yatakayofanyika Aprili 12, wilayani Monduli katika kijiji cha Enguik Monduli Juu alikozaliwa na kuzikwa.


Mbio hizo za umbali wa Kilomita 10 na kilomita 2 kutembea na kukimbia maandalizi yake kwa mujibu wa Waratibu wake mpaka sasa zimeshafikia hatua nzuri na kwa mujibu wa Waratibu wake, hatua zinazofanyika ni kufanya mazungumzo na Mgeni Rasmi ambaye kuna uwezekano akawa mmoja wa viongozi wakuu wa taifa hili.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...