Mshindi
wa Tuzo ya Media ya Awards kutoka mkoa wa Arusha(katikati) akiwa na
wenzake baada ya kutangazwa mrembo wa Vyombo vya Habari vya SJMC Radio,
Tv na Magazeti, hafla ambayo imefanyika kwenye ofisi za Chuo Kijitonyama
jijini Dar es salaam. Fainali za Miss Utalii zitafanyika tarhe
6/4/2012/13 katika Viwanja vya Makumbusho.
Mshindi
wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award kutoka Mkoa wa Arusha
Rose Godwin akikabidhiwa ua na Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya chuo cha
uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma Drk. Herbert Makoye
Mshindi
wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award kutoka Mkoa wa Arusha
Rose Godwin akivalishwa Skafu maalum ya ushindi na Mwalimu Mkuu wa
Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye
Mshindi
wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award kutoka Mkoa wa Arusha
Rose Godwin, Akiwa anasogea Mbele Mara Baada ya Kutangazwa kuwa ndiye
mshindi wa Tuzo hiyo.
Mshindi
wa Tuzo ya Miss Utalii Tanzania 2012/13-Vipaji aliye vaa Skafu ya
Tanzania wa Pili kutoka Kushoto Marry Rutta Miss Utalii Tanzania kutoka
Mkoa wa Manyara, Akiwa Mshindi
wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award kutoka Mkoa wa Arusha
Rose Godwin wa tatu kutoka kushoto, pamoja na washiriki wengine.
Mwalimu
Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert
Makoye akimtangaza Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media
Award kutoka Mkoa wa Arusha Rose Godwin.
Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award nafasi ya pili kutoka Mkoa wa Rukwa Neema Kafanunzi Akikabidhiwa Zawadi ya Ua na Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye
Mshindi
wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award nafasi ya Tatu Baby
Juma kutoka mkoa wa Mtwara Akikabidhiwa Zawadi ya Ua na Mwalimu Mkuu wa
Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye
Washiriki
wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakiwa katika picha ya pamoja Mara
baada ya kutangazwa kwa Mshindi wa tuzo ya SJMC Media Award
Rais
wa Miss Utalii Tanzania Ndugu Erasto G. Chipungahelo akitoa neno la
Shukurani kwa Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari
SJMC, Drk. Herbert Makoye ofisini kwake
Jopo la majaji wakiwa katika Picha ya Pamoja
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakitumbuiza Ngoma za asili wakati wa utoaji wa Tuzo hiyo.
Washindi sita wakiwa katika Picha ya Pamoja
Mwalimu
Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert
Makoye (wa pili kulia), akiwa na Washindi wa watatu wa Tuzo ya Media
Awards ya chuo hicho, katikati ni mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo kutoka
katika Mkoa wa Arusha.
Meneja
vyombo vya habari vya Mlimani-Mama Edda Sanga(kati) Susanne
Mbise(kushoto)na Afisa Masoko wa SJMC Sophia Ndibalema(kulia) wakiwa na
Mshindi wa Miss Utalii Tanzania-Tuzo ya Media Awards kutoka mkoa wa
Arusha, muda Mfupi baada ya kutangazwa katika Hafla iliyofanyika katika
Chuo cha SJMC.
Rais
wa Miss Utalii Tanzania wa Kwanza kutoka upande wa kushoto Ndugu Erasto
G. Chipungahelo Akiwa Na washindi watatu pamoja na Mwalimu Mkuu wa
Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye
**************
Fainali
za Utalii Tanzania zimeendelea kushika kasi kwa warembo kushindania
Tuzo mbalimbali za Utalii, Utamaduni, Jamii na za Kuichumi. Jana
lilifanyika Shindano la kumpata Mshindi wa Tuzo ya Habari (Media
Award) , Shindano ambalo liloifanyika katika Viunga vya Chuo Kikuu cha
Dar es salaam , Shule kuu ya uandishi wa Habari na Mawasiliano ya umma
(SJMC) ambao ni wadhamini wakuu wa Tuzo hiyo.
Katika
Shindano hilo la Miss Utalii Tanzania 2012/13 Media Award zaidi ya
Warembo 30 walipanda jukwaani kwa kuelezea mada ya vivutio vya Mikoa
wanayo wakirisha na kisha Majaji wa Shindano hilo kutoka Shule Kuu ya
Waandishi wa Habari na mawasiliano ya Umma walitangaza warembo Sita
walioingia katika Sita Bora na Baadae waliulizwa Maswali kila mmoja na
swali lake na pia swali la pili lilikuwa ni Swali la Jumla ambapo wote
waliulizwa.
Washiriki
wote walijibu kwa umahiri na baadae wakapatikana washindi watatu ambapo
Mshindi wa kwanza alikuwa ni Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa
wa Arusha Rose Godwin, Mshindi wa Pili alikuwa Miss Utalii Tanzania
2012/13 kutoka Mkoa wa Rukwa Neema Kafanunzi na Mshindi wa tatu
alikuwa Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Mtwara Baby Juma.
Mshindi
wa Tuzo hiyo ya Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media
Award kutoka Mkoa wa Arusha Rose Godwin Alipata zawadi ya Udhamini wa
kusomeshwa katika Shule Kuu hiyo ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano
ya Umma.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari mara baada ya kutoa Tuzo, Rais wa Miss Utalii
Tanzania aliwashukuru wadhamini wakuu wa Tuzo hiyo ya SJMC Miss Tourism
Tanzania 2012/13 Media Awards, ambao ni Shule Kuu ya Uandishi wa Habari
na Mawasiliano ya Umma kwa kutoa Heshima kubwa ya Kumsomesha Mshindi wa
Tuzo hiyo katika chuo hicho na kuongeza kuwa Elimu ndio Ufunguo wa
Maisha na Hilo ni Jambo muhimu katika Taifa letu la Tanzania ambapo
Wasomi zaidi wanahitajika ili Kujenga Taifa na Kukuza Uchumi wa nchi
yetu.
No comments:
Post a Comment