Kampuni changa ya Bigright Promotion inaanzisha
mkakati wa kuwapiganisha mabondia kwa
ajili ya kugombania mikanda au kutetea mikanda yao isipotee.Ibrahim kamwe
kiongozi wa kampuni hiyo alisema ” Tutaanzia kwa kuandaa ubingwa wa mapambano
ya uzito mdogo kabisa yaani light fly weight,baadae tunawaandalia fly weight na
super fly ,bantam …. .. ..mpaka heavy
weight ,hiyo itawasaidia mabondia kupata mapambano ya mara kwa mara na
kuwapatia kipato kidogo kwa ajira walioichagua inayoambatana na utambulishaji
wa kimataifa kwa nchi yetu,kwani mchezo wa ngumi ni mchezo mmojawapo unaoutangaza na kuipeperusha vema
bendera ya nchi yetu kimataifa,bila ya watanzania wengi kulifahamu hilo ,hivyo
kukosa usaidizi mzuri toka serikalini na taasisi binafsi tofauti na baadhi ya
nchi za wenzetu zinazopenda na kuithamini michezo, Nchi nyingi zinatangazika kupitia michezo hadi sisi tunazifahamu na
kuzitembelea au kuwa na shauku ya kutaka
kuzitembelea, wakati uwezo huo wa kufanya vizuri tunao lakini hatusaidiwi kujinyanyua wala
kuwa na sehemu ya kueleweka kwamba hii ni kwa ajili ya ngumi (ulingo wa kisasa
na ukumbi wa uhakika),na wakati wadau wa mchezo huu tunanung`unika na kuhaha
kutafuta wadhamini nasi tujikwamue
tokakatika hali tuliyonayo, kuna wengine wasio wastaarabu watataka kuchukua nafasi hii kufanya
ubadhilifu dhidi ya wanaosaidia-hii sio njema
na inadumaza michezo.
Kwa mfano
mashindano yaliyo andaliwa na bigright tarehe 7 april mwananyamala hayana
udhamini wala ufadhili wowote hivyo yanaendeshwa katika hali ya ugumu ili
vijana nao wapate kucheza kuliko kufanya mazoezi ya muda mrefu bila mashindano
hivyo kuwasababisha baadhi ya mabondia kukata tama na kuacha ngumi au
kijiingiza katika vitendo vya ukabaji jambo ambalo sio jema na laweza kuepukika
kwa kuwaandalia mashindano kama haya na ili azma yetu ya kuyafanya yaendelee
yatubidi tushirikiane kwa kushawishi wafadhili, wadhamini au wapenda mchezo
wenye uwezo kidogo wawe wanatuwezesha japo kidogo walichonacho ili nasi tuwe
tunaongeza nguvu ya kupigania michezo isidorole, mipango ikienda kama tulivyopanga tunategemea
kila mwezi kuwashindanisha kugombania ubingwa na kila mwezi wa 12 kunakuwa na
ligi ya mabingwa na kumzawadia mshindi
kitu ambacho atakuwa anakikumbuka katika maisha yake,hivyo kwa alie tayari na mwenye mapenzi na
maendeleo ya michezo tunaomba mchango wako uwe wa vifaa kama
gloves,bandages,ballguard, headguard,gumshield,chakula ,nauli,ulingo na mengineyo
mengi tu sijayaorodhesha,msitutenge na uwezo wetu mdogo tusaidiane
IBRAHIM ABBAS KAMWE
No comments:
Post a Comment