Herbert Quartey wa Ghana
Mabondia kinda Albinus Felesianu wa
Namibia na Herbert Quartey wa Ghana wanaogombea ubingwa wa dunia katika uzito wa bantam kwa vijana
kesho, watapima uzito leo asubuhi katika ofisi za bodi ya mieleka na ngumi ya
Namibia zilizoko katika eneo la katikati ya jiji la Windhoek, Namibia.
Mpambano
huo unategemewa kuwa na kila aina na hamasa kutokana na mabondia wote kuwa
wajuzi wa kuzipiga katika maisha yao mpaka sasa. Mshindi wa mkanda huu ndiye
atakayekuwa bingwa wa dunia kwa vijana katika uzito wa bantam.
Wananchi
wengi wa Namibia na kutoka katika nchi jirani kama Afrika ya Kusini, Zambia, Botswana
na Angola wameshaingia katika jiji la Windhoek na tayari hoteli na nyumba
nyingi za kulala wageni tayari zimeshajaa.
Mpambano
huu utafanyika katika hoteli maarufu ya Windhoek Country Club and Casino mahali
ambapo ni wiki moja tu iliyopita kuliwako na hekaheka nyingine ya kugombea
mkanda wa IBF wa kimataifa kati ya mabondia Immanuel“Prince” Naidjala (Namibia)
na Lesley Sekotswe (Botswana) ambao walitoka sare.
No comments:
Post a Comment