Katika picha: Samed Yesil, Jordan Ibe, Kristoffer Peterson, Craig Roddan, Ryan McLaughlin na Jack Dunn. |
Wachezaji vijana wa Liverpool wameonyesha upendo na kuguswa na watoto walioko mahospitalini katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu ya Pasaka.
Kama inavyofanywa na watu mbalimbali nyakati kama hizi za sikukuu ya Pasaka na wao pia wamewatembelea watoto na kuwapa zawadi katika hospitali iliyoko karibu na klabu yao ya Liverpool.
Jumla
ya vijana wa klabu hiyo kumi na moja kutoka katika kituo cha kukuzia
vipaji cha klabu hiyo, wametembelea hospitali ya Alder Hey jana na
kuzungumza na watoto ambapo wataendelea kuwepo hospitalini hapo kipindi
chote za sikukuu ya Pasaka.
Mlinzi
Conor Coady mwenye umri wa miaka 20, ambaye alikuwepo katika kikosi cha
kwanza cha Liverpool katika mchezo dhidi ya Anzhi Makhachkala katika
michuano ya Ulaya 'Europa League' naye alikuwa ni miongoni mwa hao
waliofanya ziara hiyo.
Amekaririwa akisema kinda huyo akisema, ‘Kufanya ziara kwa watoto hao ilikuwa jambo kubwa'.
Ameendelea kwa kusema, ‘Nina
wadogo zangu nyumbani kwa hiyo najua nini maana ya watoto hawa kupata
ujio wetu hususani kwa kuwapa faraja katika kipindi hiki.’
Wachezaji hao waligawanyika katika makundi ili kutoa nafasi ya kuzungumza watoto wengi zaidi pamoja na familia zao.
Coady
aliuungana na kundi lililokuwa likitoa zawadi ya Chocolate akiwa na
wachezaji wengine Lloyd Jones, Jordan Ibe, Ryan McLaughlin, Jack Dunn,
na Brad Smith.
Pia
alikuwepo Samed Yesil, ambaye mpaka sasa ameshaichezea ligi ndogo ya
Capital One michezo miwili kama ilivyokuwa Kristoffer Peterson, Danny
Ward, Adam Morgan na Craig Roddan.
Alder Hey Children’s NHS Foundation Trust ni
moja kati ya vituo vya afya vinavyokusanya watoto wengi barani Ulaya
ambapo watoto zaidi ya laki mbili hupatiwa huduma kila mwaka.
No comments:
Post a Comment