Wachezaji wa Azam wakijifua mjini Monrovia, Liberia |
Wachezaji wa Azam wakijifua nchini Liberia |
KOCHA Mkuu wa klabu ya Azam, wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Stewart Hall ametangaza silaha zake zitakazoshuka dimbani jioni hii katika pambano lao dhidi ya wenyeji wao Barrack YC II kuwania taji la Kombe la Shirikisho Afrika.
Kwa mujibu wa akaunti ya klabu ya Azam, ambao watashuka dimbani saa 1 jioni kwa saa za Afrika Mashariki sawa na saa 10 jioni za Monrovia, golini kama kawaida atakuwa Mwadini Ali akisaidiwa na 'kiraka' Himidi Mao na Waziri Salum upande wa kushoto na mabeki wa kati watakuwa David Mwantika na Jockins Atudo.
Dimba la kati lenyewe litashikiliwa na Michael Balou na Ibrahim Mwaipopo, huku Kipre Tchetche John Bocco, Humphrey Mieno na Mcha Khamis 'Vialli' wataongoza safu ya ushambuliaji.
Kikosi kamili cha Azam ambacho kimeapa kufa na kupona kuweza kuitoa kimasomaso Tanzania baada ya kupoteza wawakilishi wake wengine ni kama kifuatavyo;
Mwadini Ali, Himidi Mao, Waziri Salum, David Mwantika, Jockins Atudo, Michael Bolou, Kipre Tchetche, Ibrahim Mwaipopo, John Bocco, Humphrey Mieno, Mcha Khamis.
Wachezaji wa akiba; Aishi Salum, Malika Ndeule, Luckson Kakolaki, Abdulhalim Humud, Abdi Kassim, Jabir Aziz, Seif Karihe.
No comments:
Post a Comment