Mwimbaji
wa nyimbo za injili, Solomon Mukubwa, akihojiwa na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya kushiriki
katika Tamasha la Pasaka, ambapo katika Tamasha hilo mgeni rasmi
anatarajia kuwa Waziri Mkuu Peter Pinda.
Mwimbaji
wa nyimbo za injili, Faraja Ntaboba, akiimba kwa hisia moja ya nyimbo
zake mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Kamati Maalumu inayoratibu tamasha hilo la kimataifa, Alex Msama
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu
maandalizi ya tamasha hilo.
**********************************************
Na Mwandishi wetu, Dar
WAKATI
muimbaji Sipho Makhabane wa Afrika Kusini akitarajiwa kutua nchini siku
ya Ijumaa wiki hii, waimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya na
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamewasili jana jijini Dar es
Salaa, tayari kwa ajili ya kushiriki katika Tamasha la Pasaka,
litakaloanza Machi 31 kwenye Uwanja wa Taifa jijini.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Kamati Maalumu inayoratibu
tamasha hilo la kimataifa, Alex Msama aliwataja waimbaji waliowasili
jana kuwa ni Solomoni Mukubwa (Kenya) na Faraja Ntaboba (DRC).
Msama
aliwataka wapenzi, mashabiki na wadau wa muziki wa injili kujitokeza
kwa wingi katika tamasha hilo, ambalo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu
Mizengo Pinda, ili kuunga mkono juhudi za kampuni yake kuandaa tamasha
hilo kwa malengo mbalimbali ikiwemo kueneza injili ya Mungu na kusaidia
makundi maalumu.
Kuhusu
waimbaji, Msama alisema kuwa hadi kufikia Ijumaa, wakali wote wa nyimbo
za injili kutoka nje watakuwa wamewasili jijini tayari kwa tukio hilo
linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Dar es Salaam na mikoa yote
ambayo tamasha huilo litarindima.
Aidha,
mkali wa aina hiyo ya muziki kutoka Kenya, Mukubwa, alisema kuwa
amejiandaa vya kutosha katika tamasha la mwaka huu ambalo limebeba
ujumbe wa Upendo na Amani.
“Wakati
wa Uchaguzi wa Nchini Kenya tuliimba na kuhamasisha Amani na Upendo na
kwa kupitia tamasha hili tutaimba nyimbo za kuhamasisha Amani na Upendo
hapa Tanzania,” alisema Mukubwa.
Naye
mwimbaji kutoka DRC, Ntaboba alisema kuwa, watu wajitokeze kwa wingi
katika tamasha hilo na kupata burudani itakayokwenda sambamba na
mafundisho ya dini.
Msama
aliongeza kuwa idadi ya waimbaji imeongezeka baada ya kujitokeza kwa
nyota mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Ntutuma kutoka Kenya, ambapo
baada ya tamasha hilo kutikisa kwenye jijini Dar es Salaam, itakuwa zamu
ya Dodoma, Iringa, Mbeya, Mwanza kabla ya mashambulizi kuhimishwa
mkoani Mara.
No comments:
Post a Comment