Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, March 27, 2013

(COMMUNITY CENTRES) VITUO VYA KIJAMII BADO VINAHITAJIKA KATIKA MAENDELEO YA JAMII YETU


Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii wakiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya Maafisa Habari kutoka sekta mbalimbali wakiwa kwenye warsha,wakijadiliana na kutafuta  njia   mbadala itakayosababisha wananchi kujua mambo mbalimbali ya kimaendeleo  ya nchi ili kujua hali halisi ya uchumi wa nchi inavyoendelea na mengineyo.
Pichani ni baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii wakijadiliana moja ya mada iliyohusu haia ya kurudisha vituo vya kijamii (Community Centres),katika masuala mazima ya kuilemisha na kuifahamisha jamii mambo mbali yakiwemo ya kimaendeleo,Warsha hiyo ilifanyika kwa  kwa hisani kubwa ya kitengo cha mawasiliano cha wizara ya fedha na wanahabri wengine wakiwemo wa mitandao ya kijamii,ambapo mijadala mbali mbali ya jinsi ya kuwasiliana na wananchi wa kawaida   ilikuwa ikijadiliwa.

Na Ahmedy Michuzi - Jiachie Blog.
Ipo haja ya kurudisha vituo vya kijamii ( Community Centres). Ipo haja ya kurudisha vituo vya kupashana habari vya kijamii(Community Centres) ili kuboresha utaratibu wa wananchi wa kawaida kupata taarifa za kimaendeleo kwa wakati muafaka. Tangu kuondoka kwa utaratibu wa vituo hivi ambavyo vilikuwa vikisaidia kuwapasha wananchi walio mbali na miji, taarifa mbali mbali kuhusiana na maendeleo ya nchi, kumekuwa na hali ya sintofahamu zinazopelekea wananchi hawa kupotoshwa na wanasiasa na kusababisha wananchi hawa kutokuwa na imani na serikali.

Zamani, wananchi walikuwa wakivitumia vituo hivi ambavyo vilikuwepo katika kila kata, hata kwa kuangalia tu taarifa za habari na vipindi mbali mbali vya kimaendeleo, jambo ambalo siku hizi halipo kabisa. Hii ni moja ya hoja iliyojadiliwa na wamiliki wa mitandao ya kijamii kwa kushirikiana na kitengo cha mawasiliano cha wizara ya fedha ambapo, mijadala mbali mbali ya jinsi ya kuwasiliana na wananchi wa kawaida ilikuwa ikijadiliwa.

Katika Warsha hiyo ya siku ambayo pia ilihudhuriwa na maafisa habari kutoka sekta mbali mbali za kimaendeleo, wadau walikuwa wakitafuta njia mbadala itakayosababisha wananchi kujua mambo mbalimbali ya kimaendeleo  ya nchi ili kujua hali halisi ya uchumi wa nchi inavyoendelea. 

Akifungua mjadala, Ingiahedi Mduma, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano cha  Wizara ya fedha, amesema taarifa za kimaendeleo za nchi ni haki ya kila mwananchi kujua na ndio maana sasa wameamua kukaa chini na kuumiza kichwa katika kutaka kujua jinsi ya kuwafikia asilimia kubwa ya wananchi, mijini na vijijini. Warsha hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro Parh Hotel, maeneo ya Misugusugu, wilayani Kibaha, mkoa wa Pwani ambapo pia mikakati mbali  mbali ya kimaendeleo ilijadiliwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...