Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige
ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akimkabidhi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Frida
Mokit msaada wa mablang’eti ya kujifunikia wagonjwa waliolazwa Hospitalini
hapo.
Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige
ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akiwajulia hali wagonjwa
waliolazwa Hospitali ya Mt. Meru ya jijini Arusha na kuwapa zawadi mbalimbali.
Ilikuwa ni uchungu sana kwa Mbunge wa
Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine
Foundation, alipopata taarifa za watoto zaidi ya 200 wanao lelewa katika kituo
cha Yatima cha Faraja mjini Arusha. Watoto hao ni yatima ambao walitelekezwa na
wazazi wao maeneo mbalimbali mjini humo na wengine ni waathirika wa Virusi vya
Ukimwi. Mtoto aliyempakata alitupwa jalalani na wazazi wake angali mchanga na
kulelewa hadi umri huo Hospitalini hapo.
Mbunge Catherine Magige ambaye ni
Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akimkabidhi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Frida
Mokit msaada wa vitu mbalimbali kwaajili ya wagonjwa waliolazwa Hospitalini
hapo.
Wanachama wa CCM na Taaasisi ya Catherine
Foundation Development inayoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum Arusha, Catherine
Magige wakiwa wamebeba zawadi mbalimbali wakielekea katika moja ya wodi za
akina mama na watoto Hospitali ya Mount Meru jijini Arusha kukabidi zawadi
hizo.
Mbunge
Catherine Magige akiongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Frida
Mokit wakifutana na wana Catherine Foundation wakielekea kwenye moja ya
wodi za wagonja hospitalini hapo kutoa misaada.
Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige
ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akiwa amewapakata watoto
wawili mapacha waliozaliwa katika Hospitali ya Mount Meru jijini Arusha.
Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige
ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akisoma taarifa yake na
kuzungumza na watu mbalimbali wakiwapo wafanyakazi wa Hospitali ya Mount Meru.
No comments:
Post a Comment