Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya Advanced security Limited imeingia makubaliano na bingwa wa dunia
wa mchezo wa Kareti, Profesa Maurizio Martina wa Italia kwa ajili ya
kutengeneza filamu mbalimbali pamoja na ile inayopinga mauaji ya
walemavu wa ngozi, albino na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake.
Makubaliano
hayo yalifanyika jana kwenye hotel ya JB Delmonte na filamu hiyo
itaanza kurekodiwa ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa na kukamilika kwa
miezi mitatu.
Mwenyekiti
wa Kampuni ya Advanced Security Limited, Juma Ndambile alisema
kuwa sababu kubwa ya kuingia katika masuala ya filamu ni moja ya
shughuli zake katika kujihusisha na masuala ya jamii.
Ndambile
alisema kuwa kampuni yao ni Limited na kutokana na hilo inaweza kufanya
shughuli nyingine mbalimbali tofauti na huduma ya ulinzi na usalama.
Alisema
kuwa katika filamu hiyo, atawashirikisha waigizaji mbali mbali wa hapa
nyumbani na wapo mbioni kukamilisha taratibu zote kwa mujibu wa sheria
ya kurekodi filamu hapa nchini.
Kwa
mujibu wa Ndambile, Profesa Maurizio ambaye ameigiza filamu nyingi
katika nchi za mbali mbali pamoja na Uingereza na Marekani mbali ya
Italia atashirikiana na mke wake, Angel Howel na mwanaye, Dumiano ambaye
amewahi kuigiza na mcheza filamu maarufu duniani.
Profesa
Maurizio alisema kuwa pia atafundisha wanawake jinsi ya kujilinda kwa
kutumia mchezo wa karate ili kuondoa unyanyasaji wa wanawake nchini.
Amesema kuwa amefanya kazi hiyo nchi mbali mbali ikiwa pamoja na DR Congo na Afrika Kusini.
“Lengo
la filamu yangu ni kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na mila potofu za
kuwaangamiza albino na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake,”
alisema Profesa Maurizio ambaye pia ni Rais wa Dunia wa Shirikisho la
Mchezo wa Kareti.
No comments:
Post a Comment