Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, April 30, 2013

MABONDIA WATUNISHIANA MISULI KUZIDUNDA KESHO KWENYE MEI MOSI PTA SABA SABA


Bondia Amosi Mwamakula kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Rais wa IBF Africa Onesmo Ngowi katikati akionesha mzani waliopimia mabondia Thomasi Mashali kushoto na Fransic Cheka kulia katikati ni Promota wa mpambano huo Adamu Tanaka picha na mpambano wao utakaofanyika siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Amosi Mwamakula kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Yusuph Jibaba kushoto akitunishiana misuli na Shabani Mhamila 'Star Boy' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa mei mosi utakaofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akipimwa afya katikati ni mpinzani wake Amosi Mwamakula picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' akipimwa Afya leo kwa ajili ya mpambano wake
Bondia Amos Mwamakula akipimwa Afya
Baadhi ya mabondia watakaopambana kesho wakiwa katika picha ya poz wa pili kushoto ni Thomas Mashali,,Shabani Mhamila 'Star Boy' Ibrahimu Class' King class Mawe' wengine ni wapambe wao katika mchezo huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bigright amrudisha kaseba Ulingoni



bondia kamandawamakanda kushoto akitunishiana misuli na ibrahim maokola baada ya kusaini pambano lao
bingwa wa kike na msaidizi wa promota pendo njau akisimamia zoezi la usainishaji wa mikataba ya mabondia,likiwemo pambano la kuondoa utata kati ya kamanda na maokola,.bigright jafet kaseba na mabondia wengi walishuhudia

Bondia jafet kaseba anategema kupanda tena ulingoni mwanzoni mwa mwezi wa sita kuzipiga na bondia toka kenya joseph magudha katika mpambano wa kimataifa. hivyo maandalizi yamekwishaanza kwa kuwaanda mabondia watakaocheza utangulizi,kwa kuweka mapambano makali likiwemo la kamanda wa makamanda atakaezipiga na ibrahim maokola. mwanzoni maokola alikuwa amepangwa azipige na bondia toka moro na kamanda kupewa bondia mwingine, lakini kulitokea kupishana kwa maneno kati ya mabondia hao kiasi cha kutaka kupigana kavu, mabondia na viongozi waliokuwepo hapo akiwemo ibrahim kamwe walipendekeza ibadilishwe wapinzani na wawili hao wazipige kukata ngebe na majigambo ya ubabe waliyokuwa wakitupiana.mpaka sasa mapambano ya utangulizi inategemea kuwa juma seleman atazipiga na issa omar,juma fundi atapigana na moro best, yohana mathayo atazipiga joseph onyango toka kenya. na mapambano mengine yatajulishwa hapo baadae zoezi la usainishaji mikataba likikamilika

GRANDMALT EXCEL YAPAGAWISHA VYUO VIKUU DODOMA


Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Dodoma na St Johns vya mjini Dodoma wakichuana vikali katika Mpira wa Netball kwenye Uzinduzi wa Tamasha la kampeni ya kinywaji cha Grandmalt ya kuwashindanisha wanafundi ili kuweza kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslimu ijulikanayo kama Exel with grandmalt, tamasha hilo lilifanyikia kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Doodoma jana. UDOM ilishinda kwa seti 17-10 za St. Johns.
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Dodoma na St Johns (jezi nyekundu) vya mkoani Dodoma wakichuana vikali katika Mpira wa Basketball kwenye Uzinduzi wa Tamasha la kampeni ya kinywaji cha Grandmalt ya kuwashindanisha wanafundi ili kuweza kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslimu ijulikanayo kama Exel with grandmalt, tamasha hilo lilifanyikia kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Doodoma jana. St. Johns ilishinda 4-3.
 Miti ikichukuliwa tayari kwenda kupandwa..
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Joh Makini akipanda Mti katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma, anaemshuhudia ni  Meneja wa Kinywaji cha Grandmalt, Consolatha Adam. Upandaji miti huo ni sehemu kampeni ya kinywaji cha Grandmalt ya kuwashindanisha wanafunzi ili kuweza kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslimu ijulikanayo kama Exel with grandmalt, tamasha hilo lilifanyikia katika viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma jana.
Mwakilishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) mkoani Dodoma, Daniel Lekey akipanda mti katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma, Upandaji mitio huo ni sehemu kampeni ya kinywaji cha Grandmalt ya kuwashindanisha wanafunzi ili kuweza kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslimu ijulikanayo kama Exel with grandmalt, tamasha hilo lilifanyikia katika viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma jana.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha  Dodoma Kitivo cha Elimu, Erick Mhongole (katikati) akisaidiana kupanda Miti katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma, na Meneja wa Kinywaji cha Grandmalt, Consolatha Adam (kushoto) na Mtaalam wa Mazingira Chuoni hapo Nikson Makundi. Upandaji mitio huo ni sehemu kampeni ya kinywaji cha Grandmalt ya kuwashindanisha wanafunzi ili kuweza kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslimu ijulikanayo kama Exel with grandmalt, tamasha hilo lilifanyikia katika viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma jana.
Waratibu wakijadiala jambo wakati wa tamasha hilo.

Meneja wa Kinywaji cha Grandmalt, Consolatha Adam, akizungumzia zoezi la upandaji miti.
 Waratibu nao wakipanda miti UDOM
Msanii wa Mziki wa kizazi kipya nchini Joh Makini akiwapagawisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mkoa wa Dodoma kwenye Uzinduzi wa Tamasha la kampeni ya kinywaji cha Grandmalt ya kuwashindanisha wanafundi ili kuweza kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslimu ijulikanayo kama Exel with grandmalt, tamasha hilo lilifanyikia katika Viwanbja vya Nyerere Square Mnini Dodoma jana

KUTOKA KWENYE VIWANJA VYA BUNGENI MJINI DODOMA LEO


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Aprili 30,2013. Katikati ni Mbunge wa Kibaha Vijijini, Abuu Hamoug Jumaa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na  na Katibu Mkuu wa Wizara ya maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi (kushoto) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dar es salaam Apprili 30,2013.
Waziri wa Maliasili na Utalii (wapili Kulia)na Naibu wake, Lazaro Nyalandu wakiteta na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maimuna Tarishi (wapili kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Nuru Milao kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 30, 2013.Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu

MECHI YA SIMBA, POLISI MOROGORO YAINGIZA MIL 18/-


 
Mechi namba 163 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi (Aprili 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kuibuka ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Morogoro imeingiza sh. 18,014,000.
Watazamaji 3,145 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 3,564,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 2,747,898.31.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 2,841 na kuingiza sh. 14,205,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 36 na kuingiza sh. 720,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 1,812,331.75, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 1,087,399.05, Kamati ya Ligi sh. 1,087,399.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 543,699.53 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 422,877.41.
LIGI KUU YAINGIA RAUNDI YA 25
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea katika raundi yake ya 25 kesho (Mei Mosi) kwa mechi tano zitakazochezwa katika miji ya Dar es Salaam, Turiani, Morogoro na Mlandizi.
Licha ya kuwa tayari Yanga imetawazwa kuwa mabingwa wa VPL msimu huu (2012/2013), mechi dhidi ya Coastal Union itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni moja kati ya zitakazovuta macho na masikio ya washabiki wa mpira wa miguu nchini.
Mechi hiyo namba 172 itachezeshwa na mwamuzi Simon Mberwa kutoka Pwani akisaidiwa na Said Mnonga na Charles Chambea wote wa Mtwara wakati mwamuzi wa mezani atakiwa Hashim Abdallah wa Dar es Salaam. Kamishna wa mechi hiyo ni David Lugenge kutoka Iringa.
Viingilio katik mechi hiyo itakayoanza saa 10.15 jioni ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 8,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mchezo.
Mtibwa Sugar itakuwa mwenyeji wa African Lyon katika mechi namba 170 itakayochezeshwa na mwamuzi Dominic Nyamisana wa Dodoma kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro. Nayo Kagera Sugar iliyo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo itakuwa mgeni wa Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam na wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 7,000 uko tayari kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Tanzania Prisons. Nayo Ruvu Shooting itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake Mabatini ulioko Mlandizi, Pwani kuikabili Oljoro JKT kutoka Arusha.
MTANZANIA APEWA ITC KUCHEZA MSUMBIJI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Yusuf Kunasa kucheza nchini Msumbiji.
Shirikisho la Mpira wa Miguu cha Msumbiji (FMF) lilituma maombi TFF kumuombea hati hiyo Kunasa anayekwenda kujiunga na timu ya Estrela Vermelha da Beira inayocheza Ligi Kuu nchini humo.
Kunasa ambaye msimu huu hakuwa na timu (free agent) amejiunga na timu hiyo akiwa mchezaji wa ridhaa (amateur). Zaidi ya wachezaji kumi kutoka Tanzania hivi sasa wanacheza katika klabu mbalimbali nchini Msumbiji.

UZINDUZI RASMI WA SHINDANO LA "REDD'S MISS TABORA 2013" WAFAANA NDANI YA UKUMBI WA FRANK MAN PALACE HOTEL


MKALA AMBAYE NI M/KITI KAMATI MAANDALIZI YA SHINDANO, AKIELEZEA UFAAFU NA TASWIRA YA MABADILIKO YA HALI YA JUU YA SHINDANO LA MISS TABORA 2013
NASSOR WAZAMBI, MJUMBE WA KAMATI YA MAANDALIZI YA MISS TABORA 2013 AKIKAZIA MIPANGO YA MABORESHO YA SHINDANO LA UREMBO MKOANI TABORA
DADAZZZ WAKIPIGA KWITO MWANZO MWISHO
AFISA UTAMADUNI MKOA WA TABORA, BW. KATUNZI AKIZINDUA SHINDANO KWA KUKABIDHI FOMU KWA MOJA YA WASHIRIKI 
BAADHI YA WASHIRIKI WALIOJICHUKULIA FOMU ZA USHIRIKI
KUSHOTO: DIANA, ZENNA (MISS SINGIDA 2012) NA KALUNDE

JAHAZI MODERN TAARAB KUUPAMBA MKESHA WA MEI MOSI NDANI YA DAR LIVE


0 maoni

WESTERN UNION YAKABIDHI ZAWADI KWA WSHINDI WA PROMOSHENI YA UEFA


  Mkuu wa Huduma za Usafirishaji Fedha wa Benki ya DTB, Chandni Jiwa (wa pili kushoto) akikabidhi tiketi ya kwenda na kurudi Uholanzi kwa Quraish Omari Shindo mmoja wa washindi wa promosheni ya Shinda Tiketi Kuona Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) iliyokuwa ikiendeshwa na Western Union katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja Masoko na Utafiti wa Benki ya Watu wa Zanzibar (TBZ), Seif Suleiman Mohammed na Meneja wa Benki ya Posta Tanzania  Tawi la Samora), Deo Kayega.
 Meneja wa Tawi la Samora wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Deo Kayega (wa tatu kushoto) akikabidhi zawadi ya king’amuzi kwa Nicetus Joseph, mmoja wa washindi wa promosheni ya Shinda Tiketi Kuona Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) iliyokuwa ikiendeshwa na Western Union katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja Masoko na Utafiti wa Benki ya Watu wa Zanzibar (TBZ), Seif Suleiman Mohammed na Mkuu wa Huduma za Usafirishaji Fedha wa Benki ya DTB, Chandni Jiwa.
 Meneja Masoko wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Andrew Chimazi (kushoto) akionyesha mfano wa tiketi ya kwenda na kurudi Uholanzi atakayopewa mshindi wa promosheni ya Shinda Tiketi Kuona Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) iliyokuwa ikiendeshwa na Western Union katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine kushoto kwake ni, Meneja Masoko na Utafiti wa Benki ya Watu wa Zanzibar (TBZ), Seif Suleiman Mohammed na Mkuu wa Huduma za Usafirishaji Fedha wa Benki ya DTB, Chandni Jiwa.
Mkurugenzi ya Kampuni ya twenty4 Brand Communications, Monte Bilal Ikoa (kushoto) akizungumza katika hafla ambayo Western Union walikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa promosheni ya Shinda Tiketi Kuona Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) iliyokuwa ikiendeshwa na Western Union, hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Dotnata awekewa sumu kwenye juice, yamwathiri, figo, mbavu na uti wa mgongo





Muigizaji wa filamu nchini Dotnata Rubagumya anadai kuwekewa sumu kwenye juice na mtu asiyemfahamu ambayo imemsababishia matatizo makubwa ya kiafya.

Amesema alianza kuhisi kupandwa na pressure ambapo alilazwa kwenye hospitali ya IMTU na kuambiwa imepanda hadi kufikia 284 huku wakimweleza huenda ni kwakuwa amenenepa sana.Baadaye alifanyiwa uchunguzi wa moyo kwenye hospitali ya Lugalo kabla ya kupelekwa TMJ kwa vipimo zaidi.

Anasema tatizo hilo lilimsabisha ashindwe kuhema, sauti kukata na mara nyingi alikuwa akitapika.

“Nimezidiwa usiku wa kuamkia Jumatano nikakimbizwa tena TMJ ndo sasa ikabidi wanichunguze kwa makini kwanini nakuwa hivi ndo wakagundua nimelishwa sumu takriban mwezi wa nane sasa huyo mtu aliyenipa sumu aliipitisha kwa njia ya juice,” amesema Dotnata ambaye kwa sasa ameokoka.

Akizungumzia sababu za kuwekewa sumu, Dotnata amesema:

“Kila mwanadamu ana mawazo jinsi anavyowaza katika akili yake labda hakupendezewa na mimi niendelea kuishi hivi, labda alifikiria akiniua mimi yeye hatokufa. Lakini natamka wazi kwamba sitokufa nitaishi ili niyasimulie mema ya Mungu. Nimejifunza mtu anaweza kuwa rafiki yako kumbe ndio mbaya wako siwezi kujua ni kwasababu gani, namwachia Mungu.”

Monday, April 29, 2013

MAZOEZI YA MISS KIBAHA YAPAMBA MOTO

Mkufunzi wa Warembo wa Miss Kibaha Rehema Uzuwiya akizungumza na warembo hawo wakati wa mazoezi yao yanayo endelea katika ukumbi wa Vijana Kinondoni picha na www.burudan.blogspot.com

Warembo wa miss kibaha wakiwa katika pozi wakati wa mazoezi yao

Warembo watakao wania taji la Miss Kibaha wakiwa katika pozi wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika ukumbi wa vijana Kinondoni Dar es salaam picha na www.burudan.blogspot.com

WASANII BONGO FLEVA WAFUNIKA KAMPENI YA AIRTEL YATOSHA JIJINI MWANZA

  


 Ney wa Mitego, The True Boy himself.
 
WASANII wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva)  wamefunika kwa kutoa burudani ya nguvu kwenye kampeni inayoendeshwa na Kampuni ya Airtel nchini ya airtel yatosha  na kuwapa raha maelfu ya wapenzi wa muziki huo waliofurika katika  viwanja vya wazi vya Furahisha Jijini Mwanza.

Kampeni hiyo ya siku mbili iliyofanyika katika viwanja hivyo na kushuhudia na maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza kupata ushuhuda wa Airtel yatosha kwa kununua laini za simu za mkononi za Kampuni hiyo na jinsi ya kutumia huduma ya Internet, kuongea kwa kujiunga na kupata dakika nyingi za muda wa maongezi kwenda mitandao mingine kwa bei nafuu zaidi kwa laini moja tu ya Airtel.

Wasanii wa Bongo Fleva waliotoa burudani na kuwaacha hoi maelfu ya wananchi waliofurika kupitia vibao vyao vinavyotamba kwenye vituo mbalimbali vya redio na televisheni hapa nchini ni pamoja na Juma Kassim ‘Nature’ na kundi lake la Wanaume Halisi, Roma Mkatoliki, Madee na Ney wa Mitego.

Maelfu ya wananchi walioshuhudia kampeni hiyo waliweza pia kushuhudia vipaji vya uimbaji kutoka kwa vijana walioshindanishwa na waliojitokeza kucheza muziki wa Bongo fleva katika viwanja hivyo na
kupata zawadi ya laini na fulana (T-shirt) za Kampuni ya Airtel zilizotolewa kwa washindi waliopatikana.

“Wananchi wengi wamekuja hapa kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongo fleva kama ulivyojionea lakini pia wengi kwa sasa wanatumia mtandao wa Airtel ikiwemo huduma hii ya Airtel yatosha pamoja na kununua laini na kupatiwa maelezo ya jinsi ya kutumia huduma hii”alisema msanii Ney wa Mitego.

Akizungumzia Kampeni hiyo Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Jackson Mmbando alisema kwamba tangu kuzinduliwa na kufanyika  katika mikoa sita hadi sasa hapa nchini kumekuwa na mapokeo na mafanikio makubwa kwa kuongeza wateja wanaotumia mtandao wa Airtel kupitia huduma zote.

Mfanyabiashara wa vituo vya kuuza mafuta Barnabas Mathayo wa Jijini Mwanza alitoa ushuhuda wa kukubali huduma inayotolewa na Airtel katika mahojiano maalumu alisema kwamba tangu kuanzishwa kampeni ya Airtel yatosha amekuwa akinunua kifurushi na kujiunga na kujipatia muda wa kutosha kufanya mawasiliano na ndugu, rafiki, wavuvi wanao nunua mafuta kwaajli ya boti zao pamoja na wafanyabiashara mbalimbali kupitia mitandao yote kwa bei ile ile.
 
“Huu ni Mkoa wa sita sasa na kama mlivyoshuhudia wingi wa watu wanaokuja kushuhudia burudani na kupata maelezo ya jinsi ya kutumia mtandao huu kwa garama nafuu zaidi na ikizingatiwa Mkoa wa Mwanza ni moja ya mikoa inayojishugulisha na uvuvi, kilimo, ufugaji na wafanyabiashara kutoka ndani na nchi za maziwa makuu”alisema Meneja huyo.

“Hatukaangi laini ni moja tu yatosha zingine za nini na ukiangalia Mwanza ni Mkoa wa burudani, biashara, viwanda, kilimo, uvuvi na ufugaji hivyo wananchi wake hawana budi kutumia mtandao wa Airtel ambao umedhamiria kuwainua kiuchumi na kuletwa kwa kampeni hii itawasaidia kujifunza Airtel kuna nini ndani ya mtandao huu”alisema

Mbando aliongeza kuwa kampeni hiyo inaendelea katika Mikoa ningine na mwishoni mwa juma hili kampeni hiyo itahamia Jiji kubwa la Dar es salaam katika viwanja vya Zakhem na kutakuwa na burudani ya kukata na  shoka kutoka kwa wasanii mbalimbali kutokana na wasanii wengi kuwa jijini humo na kutoa wito kwa wananchi kufika kushuhudia na kujifunza ndani ya mtandao wa Airtel kuna vitu gani na kwa gharama nafuu.
 Mashabiki wa True Boy, Ney hawakuwa nyuma
 Msanii Chipukizi aliyeonyesha kipaji cha hali ya juu kwa kughani mashairi yenye mvuto kwa miondoko ya HIPHOP wa mkoani Mwanza maarufu kwa jina la Dogo D alifanya burudani kali katika tamasha maalum la
Airtel yatosha mkoani Mwanza katika viwanja vya Furahisha
Ujumbe kutoka kwa wananchi unasomeka
 Roma kazini
 Roma Mkatoliki, baada ya kuwatosheleza kwa burudani wakazi wa Mwanza
Madee kutoka Manzese...
 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...