Na Mahmoud Ahmad, Arusha
Siku
chache tu baada ya taifa kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa
waziri mkuu nchini, Edward Moringe Sokoine aliyekuwa mwenyekiti wa Uvccm
mkoani Arusha, James Ole Milya ameibuka na kutamka kwamba jamii ya
kimasai imetupwa na kubaki kama yatima ndani ya nchi yao.
Ole
Milya, alitoa kauli hiyo juzi wakati akizuru kaburi la hayati Sokoine
ambapo akiongea na waandishi wa habari alitamka kwamba serikali
haimuenzi kiongozi huyo kwa vitendo na badala yake imekuwa ikipora haki
za wafugaji kwa kumega ardhi yao kila kukicha.
Alisema
kuwa tangu kufariki kwa Sokoine ambaye alikuwa msatari wa mbele
kupigania haki za makabila yote nchini lakini kwa hali ya sasa jamii ya
kimasai imetupwa na vijana wake wamebaki wazururaji na walinzi katika
nchi yao.
“Jamii
ya kimasai inamkumbuka Sokoine kwa masikitiko makubwa sana kwani
wamebaki wazururaji na walinzi katika nchi yao”. Alisema kwa huzuni
Hata
hivyo,Ole Milya ambaye kwa sasa yuko Chadema alisema kuwa marehemu
Sokoine alikuwa ni kiongozi wa mfano kwa kuwa alitoa ushirikiano katika
maeneo mbalimbali nchini, lakini cha ajabu serikali imeshindwa kufuata
nyendo zake.
Alisema
kuwa serikali imeyasahau yote mazuri aliyokuwa akiyafanya wakati wa
uhai wake huku akisisitiza kuwa kwa hali ya sasa keki na taifa inaliwa
na watu wachache badala ya wananchi wote.
Ole
Milya alisisitiza kuwa yeye anatoka katika jamii ya wafugaji wa kimasai
na isingekuwa jitihada za wafadhili wachache ambao ni wazungu kumpeleka
shule leo angekuwa mlinzi katika nyumba za baadhi ya watanzania.
Hata
hivyo,alisema kuwa tangu kufariki kwa Sokoine ardhi ya jamii ya kimasai
imekuwa ikimegwa siku hadi siku na serikali tofauti na maeneo mengine
hapa nchini.
Alisema
kuwa wachache kama yeye wataendelea kumuenzi Sokoine kwa kusema ukweli
ndani ya nchi yao bila kujali vitisho vya kuuwawa au kuteswa.
“Nahaidi
kuishi kama Sokoine hata kama nikitolewa vitisho vya kuuwawa niko
tayari kusema ukweli bila kujali kupingwa wala kupigwa”alisema Ole Milya
No comments:
Post a Comment