DAR ES SALAAM, Tanzania
SHIRIKA
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), linatarajia kushirkiki maonesho ya
siku tatu ya Huduma za Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (The Muhimbili
Day Exhibitions 2013), ambayo yanafunguliwa rasmi kesho Jumatano na
Waziri wa Afya, Dk Hussein Mwinyi.
Maonesho
hayo yanayoratibiwa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), yatafikia
tamati Ijumaa Aprili 19, yakiwa na nia ya kutoa nafasi ya kukuza huduma
zake kwa wateja wake, kwa kushirikisha taasisi na kampuni mbalimbali
zenye udau katika sekta ya afya nchini.
Akizungumza
na Habari Mseto, Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga, alisema
walipokea mwaliko wa ushiriki wa maonesho hayo kutoka MNH na kisha
kuthibitisha, wakimiani ni fursa pana itakayotangaza huduma za shirika
hilo ambazo zina uhusiano wa karibu na sekta ya afya.
Aliongeza
kuwa, wanachama na wasio wanachama wa NSSF watapata fursa adhimu ya
kujionea utoaji na uendeshaji wa huduma mbalimbali, zilizo na udau na
Sekta ya Afya, kama vile Mafao ya muda mrefu na Mafao ya muda mfupi.
Aliongeza
kwa kuyataja mafao ya muda mfupi kuwa ni pamoja kuumia kazini, ambapo
kuna namna mbili za kuumia akizitaja kuwa ni kuumia kwa taratibu
kunakotokana na kazi husika na kuumia kwa ghafla kama vile kukatika
mkono na viungo vingine vya mwili.
Mafao
ya Uzazi kwa akina mama, mafao ya rambirambi katika mazishi ya
mwanachama, mafao ya uzeeni, mafao ya ulemavu haasa ulemavu utakaomtoa
mwanachama moja kwa moja kazini, pamoja na ya mirathi, ambapo mke/mume
na watoto ndiyo wanawajibika kumrithi mwanachama.
Maonesho
hayo ya kila mwaka yanahusisha wadau wa afya wanaotoa huduma za
matibabu na upasuaji, wataalamu wa mionzi, wafamasia, wamiliki wa
maabara, maduka ya dawa, wasimamizi wa taarifa za kitabibu na huduma
nyinginezo za kitiba.
‘Muhimbili
Day Exhibitions’ ni maonyesho yanayotoa fursa ya kipekee kwa washiriki
kuonyesha bidhaa na huduma zao, ambayo pia ni jukwaa kamili la kujenga
mahusiabno ya kibiashara kati ya watoa huduma na wateja wao, ikiwamo
kupokea maoni kutoka kwa watumiaji wa bidhaa zao.
No comments:
Post a Comment