Mwenyekiti
wa TASWA, Juma Pinto akimkabidhi Tuzo ya Mwandishi Bora wa Michezo kwa
upande wa Radio, Abdalah Majura, wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT), (Picha na Habari Mseto Blog)
DAR ES SALAAM, Tanzania
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewapongeza waandishi watatu wa habari za michezo k
Waandishi
hao walioshinda katika kategori ya michezo na utamaduni ni Abdul
Mohammed wa The African kwa upande wa magazeti na Abdallah Majura wa
redio ABM kwa upande wa redio.
TFF
tunawapongeza kwa ushindi huo uliotokana na makala zao ambazo zina
mchango katika maendeleo ya mpira wa miguu, lakini pia ni changamoto kwa
waandishi wengine ambao hawakufanikiwa kushinda.
Vyombo
vya habari vina nafasi kubwa katika ustawi wa michezo ukiwemo mpira wa
miguu, kwani katika nchi nyingine vimefichua rushwa. Ni matarajio yetu
kuwa vyombo vya habari nchini navyo vitakuwa mstari wa mbele katika
kufichua na kupambana na rushwa katika mpira wa miguu.
MECHI YA AZAM, BARRACK YAINGIZA MIL 44/-
MECHI
ya marudiano ya raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam ya
Tanzania na Barrack Young Controllers II ya Liberia iliyochezwa jana
(Aprili 6 mwaka huu) imeingiza sh. 44,229,000.
Fedha
hizo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na
kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu zimetokana na watazamaji 17,128
waliokata tiketi.
Viingilio
vilikuwa sh. 2,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000 ambacho
kilikuwa kiingilio cha juu kwa jukwaa la VIP A. Kiingilio cha sh. 2,000
ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 15,212.
Mgawo
ulikuwa kama ifuatavyo; gharama za tiketi sh. 5,575,500, asilimia 15 ya
uwanja sh. 5,798,025, asilimia 10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh.
3,865,350 na asilimia 75 iliyokwenda kwa klabu ya Azam ni sh.
28,990,500.
Mechi
iliyopita ya raundi ya awali ya mashindano hayo kati ya Azam na El
Nasir ya Sudan Kusini iliyochezwa kwenye uwanja huo huo Februari 16
mwaka huu iliingiza sh. 34,046,000 kwa viingilio hivyo hivyo huku
ikishuhudiwa na watazamaji 13,431.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment