Katika maadhimisho ya siku ya siku ya uandishi wa Vitabu na Hati Miliki
Duniani Afisa Habari wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (katika
ngazi ya Kimataifa) UNIC Bi. Stella Vuzo akizungumza na wanafunzi wa
shule mbalimbali waliohudhuria semina fupi iliyoandaliwa na UNIC na
kuwafafanulia umuhimu wa kusoma vitabu mbalimbali ambapo wanaweza
kujifunza mambo tofauti ikiwemo kujua takwimu za ugonjwa hatari wa
Malaria hapa nchini ambao umekuwa ukiongoza kwa kusababisha vifo vya
watoto wenye umri chiniya miaka 5, hivyo kwa usomaji vitabu wanaweza
kujua namna ya kujikinga na wanapogundua dalili kuweza kuwahi kupata
matibabu.
Wanafunzi
wa darasa la Saba shule ya msingi Oysterbay wakimsikiliza kwa makini
Afisa Habari wa UNIC (katika ngazi ya Kimataifa) Bi. Stella Vuzo (hayupo
pichani) wakati akielezea kazi zinazofanywa na Shirika la Afya Duniani
WHO lililochini ya Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha Ugonjwa wa
Malaria unatokomezwa duniani katika nchini za kusini mwa Jangwa la
Sahara. Ikiwa zimebaki siku mbili kuadhimisha siku ya Malaria duniani
inayodhimishwa kila mwaka Aprili 25 wakati wa siku ya kuadhimisha siku
ya uandishi wa vitabu na hati miliki duniani.
Msaidizi
wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha akiendesha chemsha bongo kwa wanafunzi
walioshiriki semina hiyo kupima uelewa wao kuhusiana na Ugonjwa wa
Malaria.
Picha
juu na chini ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Usomaji na Maendeleo Bi.
Demere Kitunga ambaye ni mmiliki wa Book Cafe iliyopo maeneo ya
Mikocheni jijini Dar akiwaelezea wanafunzi umuhimu wa kuwa na nia na
dhamira ya kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu vya nyanja mbali mbali
ikiwemo vya Kiada, Ziada na vya maarifa ambapo amewapa changamoto
kujianzisha Maktaba binafsi na vikundi ambapo wanaweza kuchangishana
fedha kidogo kwa uwezo wao ili kuweza kujinunulia kitabu ambacho
wanaweza kushirikiana kusoma ambavyo vitawapa uwezo wa kujitambua, kuwa
na maamuzi, kupata uelewa wa vitu tofauti vinavyoweza kuwajengea
kujiamini na kuwawezesha kubadilisha mfumo wa maisha katika makuzi yao.
Katibu Mkuu wa Mtandao wa Vilabu vya Umoja wa mataifa Tanzania (UNCTN)
Bernadetha Mshana akionyesha moja ya kitabu kilichomsaidia kuweza
kupata uelewa wa kuongea Kingereza kwa urahisi zaidi ikiwa ni ushuhuda
wake kwa vijana wenzake kuwa usomaji vitabu hupanua uelewa wa mtu na
kujua mambo mengi.
No comments:
Post a Comment