Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 25, 2013

CATHERINE FOUNDATION YATOA MSAADA DODOMA


Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda na Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Catherine Magige wakiwakikabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Matumaini cha mjini Dodoma.
 *****  ******
Asasi ya Kijamii ya Catherine Foundation jana imetembelea kituo cha kulelea wa watoto cha Matumaini Village kilichopo mkoani Dodoma ambapo walikwenda kutoa misaada mbalimbali wakiongozwa na Mkurugenzi wa Asasi hiyo, Catherine Magige.
Katika Hafla hiyo Mgeni Rasmi alikuwa Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda ambapo asasi hiyo ilitoa vitu mbalimbali vikiwemo, Madaftari, Mafuta, Sabuni, Juice, miswaki na dawa zake, mchele, sukari, nguo za watoto, kanga za wakinadada wanaowalea watoto hao na vingine vingi.

 
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akihutubia katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Catherine Magige akihutubia katika hafla hiyo jana.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akiwakikabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.
Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Catherine Magige akiwakiwapa zawadi mbalimbali kwa watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...