MABINTI wanaopenda kushiriki mambo ya urembo wameombwa
kujitokeza kwa wingi kushiriki shindano ya la kumsaka Redds Miss Kibaha 2013.
Akizungumza leo mchana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa
shindano hilo, Khadija Kalili alisema hadi sasa washiriki wachache
wamejitokeza na kutoa fursa ya wasichana wengine kuchukua fomu za usajili
ili washiriki kwenye shindano hilo.
Mratibu wa Miss Kibaha 2013, Khadija Kalili.
Alisema siku rasmi ya uzinduzi wa shindano hilo itatangazwa
baadaye ambapo pia washirki hao wataanza mazoezi rasmi ikiwa ni pamoja na
kutangaza pia namna ya kupatikana mrembo mwenye sifa kwa Kibaha nzima.
“Miss Kibaha 2013 inaandaliwa
na Kampuni ya Linda Media Solution (LIMSO), ambapo pia shindano hilo
litafanyika katika ukumbi wa Kontena Kibaha Maili moja.
“Natoa wito kwa wasichana wenye sifa na wanaotaka
kutimiza njozi zao kujitokeza kushiriki huku tukizingatia umri kati ya
miaka 18 hadi 24 wenye uraia wa Tanzania hiyo ikiwa ni katika hatua ya
awali ya kumpata Miss Tanzania wa mwaka huu kwani warembo wote wa Taifa
hupatikana katika hatua za mashindano ya awali.
Mbali ya kuomba warembo kujitokeza pia Kalili ameomba
wadhamini mbalimbali kujitokeza na kutoa sapoti ili kuweza
kufanikisha shindano hilo linalofanyika mara moja tu kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment