Baada
ya kukwama kwa Muda Mrefu Kutokana na baadhi ya wadhamini kushindwa
kutimiza ahadi zao za udhamini hatimaye Bodi ya Mashindano ya Miss
Utalii Tanzania imehamishia fainali hizi za Miss Utalii Tanzania 2012/13
mkoani Tanga badala ya Dar es salaam ambazo zilikuwa zifanyike awali.
Taratibu
zote za fainali za Show ya Taifa kufanyika Tanga zimekamilika ikiwemo
kukamilisha sheria ya ya uendeshaji wa Shughuli za sanaa na Fainali
za Urembo ambapo Serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa hatimae
limetoa kibali kwa fainali hizo Kufanyia Tanga tarehe 11.05.2013,
waandaaji wamewasilisha BASATA uthibitisho wa Zawadi kwa Washindi,
Pamoja na mikataba ya kulinda haki na wajibu wa waandaaji na washiriki
wa Fainali Hizo.
Hii
itakuwa ni Mara ya kwanza kwa Mkoa wa Tanga kuwa wenyeji wa Fainali za
Taifa za mashindano ya Urembo na ni mara ya pili kwa Fainali za Taifa za
Miss Utalii Tanzania Kufanyikia Nje ya Dar es salaam baada ya Fainali
za mwaka 2005 kufanyikia Mkoani Arusha.
Hii
ni Heshima na Fulsa ya pekee kwa Mkoa wa Tanga ya kuhidhilishia na
kuutangazia Ulimwengu vivutio vyake vya Utalii, Utamaduni, Uwekezaji, na
Miundo mbinu kitaifa na kimataifa. Lakini pia hii ni Fulsa kwa Jiji la
Tanga kuuthibitishia Ulimwengu kuwa Jiji la Tanga linao uwezo wa kuwa
wenyeji wa Tukio la Kitaifa. Kufanyika kwa Shindano hili Mkoani Tanga
kutasaidia pia Kuhamasisha pia Kampeni dhidiya , Uharibifu wa mazingira,
Uvuvi Haramu, Uwindaji Haramu, Tohara kwa wanawake, Utamaduni, mila na
Desturi kongwe na Potofu.Madawa ya kulevya, Rushwa, Ubaguzi wa Kijinsia,
na Mmomonyoko wa Maadili katika jamii.
Wakati
huo serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imewapongeza juhudi
zinazo fanywana Waandaaji wa Miss Utalii Tanzania za kutangaza vivutio
vya utalii na utamaduni wa Tanzania kitaifa na kimataifa kwa kuipatia
Sifa kubwa Tanzania kupitia mashindano hayo.
Kwa
mujibu wa maelezo ya Barua ya Tarehe 19.04.2013 iliyo sainiwa na Ndugu
Z. A Kimwaga kwa niaba ya Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii
kwenda kwa waandaaji wa Miss Utalii Tanzania. Wizara na serikali kwa
ujumla inatambua juhudi zinazofanywa na waandaaji wa mashindano haya
katika kukuza utalii wa ndani na Utalii wa Kitamaduni.
Katika
kuthibitisha hilo Wizara imewashauri waandaaji wa mashindano hayo
kuwaslisha maoombi ya msaada kutoka serikalini kwa wakati na kwa
kuzingatia misimu na Bajeti ta serikali ili kuwe na uwezekano wa
serikali Kudhamini mashindano hayo. Hata hivyo Serikali kupitia Taasisi
zake za Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa(TANAPA) , Mamlaka ya
Ngorongoro(NCIA), na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa miaka yote
ikiwepo mwaka huu imekuwa ikitoa udhamini wa Hali na Mali katika
kufanikisha Mashindano hayo.
Nae
Rais wa Mashindano hayo Gidion Chipungahelo kwa niaba ya Bodi ya
Mashindano amewaomba Radhi watanzania wote , wadau w ashindano ,
washiriki, wadhamini na wengine wote walioguswa au kuathiriwa kwa namna
yoyote.
No comments:
Post a Comment