SIKU
chache baada ya Mbeya yetu kuripoti habari kuhusu baadhi ya Wananchi
kulalamikia ubovu wa Barabara katika Maeneo ya Iyunga Viwandani kutelekezwa na
ngazi husika madhara yaanza kutokea baada ya magari kuanza kuanguka yakiwemo ya
Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Baadhi
ya barabara zinazo lalamikiwa na wananchi hao ni ile inayo toka eneo la Ituta
Iyunga ambayo inaelekea katika viwanda vya makampuni ya Cocacola, Pepsi, Tbl,
pamoja na kiwanda cha utengenezaji malumalu(Marmo granite limited).
Wakizungumza
na Mbeya yetu kwa sharti la kutotaja majina yao wananchi hayo walisema barabara
zinazo elekea viwandani humo ni mbovu na hazina hadhi ya kutumiwa na makampuni
hayo.
Walisema
kutokana na hali hiyo hawaoni mchango na umuhimu wa uwepo wa makampuni makubwa
maeneo yao kutokana na kushindwa kuhudumia barabara ambazo wanapitisha bidhaa
zao wenyewe.
Aidha
wameziomba mamlaka husika jijini humo kuhakikisha wanayafanyia kazi malalamiko
hayo kwani ni kero kubwa hasa katika kipindi hiki cha msimu wa mvua.
Baadhi
ya madereva wanaopita na magari ya mizigo kutoka viwandani walisema magari yao
hushindwakumudu kutokana na ubovu wa miundombinu hiyo licha ya kutoa ushuru
mkubwa kwa halmashauri ya Jiji.
Walisema
baadhi ya bidhaa wanazokuwa wamezibeba haziitaji mtikisiko mkubwa kutokana na
kupoteza ubora wake hivyo wakiendelea kupita kwenye barabara hizo kampuni
hupoteza wateja kutokana na bidhaa kupoteza ubora.
Baadhi
ya Magari yalioanza kupata madhara kutokana na ubovu wa barabara hizo ni Gari
inayomilikiwa na Kampuni ya Cokacola yenye namba za usajili T 781 ALL, yenye
Tela namba T 168 ALD likiendeshwa na dereva Medson Msisya pamoja na Gari ya
Halmashauri ya Jiji lenye namba SM 2732 lililokuwa likienda kunyonya maji
machafu katika Barabara hiyo hiyo ya Viwandani.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Juma Iddi alipoulizwa kuhusu barabara
hizo alisema Makumpuni hayo yana ubishi kwa kushindwa kufanya ushirikiano na
Halmashauri ya Jiji ambayo tayari imeshaanza kukarabati baadhi ya maeneo.
Alisema
barabara hiyo ipo kwenye kiwango cha vumbi hivyo kutokana na kupitika mara kwa
mara na makampuni hayo inabidi ipandishwe ili ijengwe kwa kiwango cha
changarawe ili zipitike kipindi chote cha Mwaka.
Iddi
alisema kutotengenezwa kwa barabara hiyo kwa sasa kumetokana na kukosekana kwa
fedha ambazo hutegemea kutoka kwenye mfuko wa barabara pamoja na fedha za
halmashauri.
Pia
alisema kwa sasa Halmashauri hiyo inasubiri fedha za mabaki kutoka Mfuko wa
benki ya dunia ambazo zinakarabati Barabara za Jiji kwa kiwango cha Lami.
|
No comments:
Post a Comment