CHAMA
cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS),kimeahidi
kusaidia masuala mbalimbali yahusiyo mafunzo kwa waandishi wa habari za
michezo wa Tanzania.
Rais
wa AIPS,Gianni Merlo raia wa Italia aliwapa fursa viongozi wa vyama vya
waandishi wa habari za michezo wa Afrika kuwasilisha changamoto
mbalimbali zinazovikabili vyama vyao, lakini kati ya hizo changamoto
waitaje moja ambayo wanataka AIPS isaidie kuwapa msaada.
Tunashukuru
Merlo kwanza alivutiwa sana na namna Chama cha Waandishi wa Habari za
Michezo Tanzania (TASWA) kinavyofanya kazi zake na ushiriki wake wa
mikutano ya Dunia mara kwa mara, hali ambayo aliahidi yeye binafsi
kusaidia chama chetu kuboresha masuala ya kimsingi.
Kubwa
ambalo AIPS baada ya kuelezwa imesema italipangia utaratibu ni suala la
mafunzo kwa waandishi wa habari chipukizi na wanawake kwani hayo ni
baadhi ya mambo ambayo wenyewe wanayatilia mkazo na hasa baada ya
kujulishwa kuwa kuna wanahabari zaidi ya 50 wanawake hapa nchini
wanaofanya kazi kwenye masuala ya michezo.
Hata
hivyo ingawa TASWA iliomba isaidiwe mafunzo kwa wanachama wake wote kwa
kupatiwa wataalamu hasa wakati huu ambao kuna changamoto kubwa ya
teknolojia ya habari na mawasiliano, lakini AIPS imesema kwa mwaka huu
uwezo wake ni kwa waandishi wa habari za michezo chipukizi kupitia
programu inayoandaliwa na AIPS.
Lakini
Rais wa AIPS aliutaka ujumbe wa Tanzania utakapokuwa umerudi nyumbani
umuandalie mikakati hiyo kwa mafunzo ya wanawake ili ikiwekezekana
yafanyike kwa awamu katika kipindi cha miezi 18 kutegemea na idadi ya
wahusika na pia gharama zenyewe. Nchi
wanachama 103 duniani zikiwemo nchi 24 za Afrika zilihudhuria mkutano
huo uliomalizika juzi Sochi, Urusi, ambapo pia ulifanyika uchaguzi wa
viongozi wa AIPS watakaokuwa madarakani kwa miaka minne ijayo, ambapo
Merlo alipita bila kupingwa.
Mkutano
Mkuu wa AIPS ambao ni wa 76 ulimalizika juzi, ambapo kulikuwa na kikao
cha makatibu wakuu wa kila nchi kilichoendeshwa na Katibu Mkuu wa AIPS,
Roslyn Morris ambapo Tanzania iliwakilishwa na Katibu Mkuu wa TASWA,
Amir Mhando na huko pia suala la tuzo mbalimbali zinazotolewa na
wanahabari zilizungumzwa kwa kina.
Pia
kulifanyika kikao cha marais wa AIPS wa mabara na baadhi ya viongozi wa
vyama vya wanahabari wa michezo wa Afrika kilichokuwa chini ya Merlo,
ambapo nilidhuria na ajenda kubwa ilikuwa suala la rushwa kwenye michezo
na mambo ya upangaji wa matokeo wa mechi mbalimbali. Baada
ya mkutano huo, wakati ujumbe wa Tanzania ukiwa njiani kurejea nyumbani
ulipitia jijini Moscow, Urusi na kuzungumza masuala mbalimbali na
Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Jaka Mwambi.
Kwa
ujumla mkutano ulikuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania na Afrika kwa
ujumla, ambapo masuala mengine mengi yaliyojitokeza kwenye mkutano huo
ikiwemo namna ya mafunzo hayo yatakavyofanyika tutayazungumza Jumatano
ijayo kwenye mkutano na wanahabari utakaofanyika ukumbi wa City Sports
Lounge, Dar es Salaam saa tano asubuhi.
TASWA
ni mwanachama hai wa AIPS yenye makao yake makuu Lausanne, Uswisi,
ndiyo sababu kila mwaka tumekuwa tukishiriki mikutano hiyo tangu
tulipoingia madarakani mwaka 2010.Mwaka 2011 tulishiriki Mkutano Mkuu wa
AIPS uliofanyika Seoul Korea, Korea Kusini na tuliwakilishwa na Makamu
Mwenyekiti, Maulid Kitenge na Katibu Msaidizi, George John
Pia
tulishiriki Mkutano Mkuu wa AIPS uliofanyika Innsbruck, Austria Januari
mwaka jana, ambapo Katibu Mkuu, Amir Mhando alihudhuria.
No comments:
Post a Comment