KAMPUNI ya Voda com nchini hivi karibuni ilianzisha huduma
ya kipekee ambayo ilikuwa inamuwezesha mtumiaji wa mtandao wa VODACOM kununua
muda wa maongezi wa mitandao mingine nchini kwa kutumia huduma za M PESA.
Huduma hii ni mapinduzi makubwa kwenye mtandao wa VODACOM
ambayo mbali ya kukuza huduma yake imeweza kuvuka mipaka na kusaidia wateja wa
mitandao mingine
Kampuni ya Vodacom ambayo kwa sasa inatamba na huduma yake
bora ya M-PESA iliyojizolea umaarufu mkubwa nchini kupitia huduma hiyo
VODACOM ambayo siku zote imekuwa karibi sana na jamii hivi
karibuni ilikuwa na huduma nyingine nzuri sana ambayo ilikuwa inamuwezesha
mteja wa M-PESA Kununua vocha ya mitandao mingine nchini hii ni huduma iliweza
kuwa ondolea adha wateja pindi wanapotaka kuwanunulia muda wa maongezi wenzi
wao ambao wapo katika mitandao mingine ili kufanya hivyo mteja wa MPESA
alitakiwa kuingia kwene menu ya Mpesa na kufuata taratibu kama afanyavyo
anapotaka kununua LUKU au huduma nyingine ila hii ni kununua muda wa maongezi
wa mtandao mwingine alipaswa kuinginza namba 484848 kama namba ya kampuni na kisha
kuingiza namba ya simu ya mtu anayetaka kumtumia mda wa maongezi kwa mtandao
wowote ule nchini kama namba ya kumbukumbu
Hakika huduma hii ni nzuri na inarahisisha maisha na
inawezesha watumiaji wa mtandao wa voda com kuwa nunulia wenzi wa
o muda wa
maongezi pasipo kujali wana tumia mtandao gani
Haya ni mapinduzi makubwa ya kutechnologia nchini na
yanapaswa kuungwa mkono na kupewa Baraka zote
Kinacho nishangaza mpaka sasa nikiwa kama mwana habari ni
kuwa mbali na huduma hii kuwa nzuri na kuwaaidia watanzania hususani watumiaji
wa mpesa huduma hii sijasikia kutangazwa
ili watanzania wote waijue na kama nionavyo mimi ambaye nimeshaitumia na
kujua uzuri wake naona ni bora itangazwe zaidi ili jamii ijue na kunufaika
nayo.
Mbali na uzuri wake na kurahisisha maisha kinacho
nistajaabisha kuwa katika siku kama mbili zilizopita nimekuwa nikijaribu
kutumia huduma hiyo na imekuwa haipatikani na jamaa zangu ambao wote tumekua
tukitumia huduma hiyo kwa pamoja tunajiuliza kulikoni nini kimetokea hadi
huduma huu nzuri ikasimama
No comments:
Post a Comment