Shirikisho linalosimamia mchezo wa mpira wa pete duniani (IFNA) limebadili jina na sasa litajulikana kama shirikisho la kimataifa la mpira wa pete
Shirikisho
hilo lenye makazi yake makuu huko umoja wa nchi za kifalme limesema lipo kwenye
kipindi cha mpito katika kuuboresha mchezo huo ambapo kitaongeza mchezo
mwingine ujuliakan nao kama Fast5 na michezo mingine ya kimaendeleo
Shirikisho
hilo limesema kuwa mabadiliko ya jina hilo kutoka IFNA hadi
INF ni kuliweka shirikisho hilo kwa ukaribu na vyama vingine vya michezo
duniani .
Aidha
shirikisho hilo limesema hata nembo ya kampuni hiyo imebadilishwa na nembo ya
sasa itakuwa inaashiria uongozi zaidi tofauti na hapo mwanzo na lengo kubwa ni
kubadili muonekano wa mpira wa pete.
Katika nembo
hiyo ya sasa inaonyesha mikono inayoshikilia mabara yote sita na kuyaleta
pamoja katika mchezo wa mpira wa pete
".
Nembo hiyo
mpya itazungushwa katika mabara yote kuashiria kuwa nembo mpya imeanza kufanya
kazi .
No comments:
Post a Comment