Wateja waBenkiya NMB wakipatamaelekezoyahudumaza JISEVIE
kutokakwaOfisawa NMB tawi la NMB House
Edith Mavura.Hudumazitolewazokwawatejawa NMB waliojisajilikutumia NMB
Mobile
.Hudumainayomuwezeshamtejakupatahudumazakibenkimahalapopotebilakufikakwenyetawi
la NMB
Wateja wa Benkiya NMB
wakipata maelekezo yanayohusu maboresho ya huduma ijulikanayo kama JISEVIE
kutoka kwa Ofisa wa NMB tawi la Bank House, Salvatory Mushi .Jisevie inamsaidia mteja wa
NMB kupata huduma za kibenki sehemu yoyote atakapokua bila kufika kwenye tawi la
NMB.Mteja ataweza kutumia simu yake ya kiganjani na kutembelea Mashine za kutoa fedha ili Kujisevia.
Ofisawa NMB tawi la Bank House, Salvatory Mushi
akimwelekeza mteja wa NMB jinsi ya kujiungana NMB Mobile ili KUJISEVIA huduma zitolewazo kwa wateja wa
NMB waliojisajili kutumia NMB Mobile .Huduma inayomuwezesha mteja kupata huduma za kibenki mahala popote bila kufika kwenye tawi
la NMB
Ofisa wa NMB tawi la
Loliondo, Lembris Lesion akimwelekeza Mchungaji mstaafu, Ambelikile Mwaisapile jinsi
ya kujiungana NMB Mobile ili KUJISEVIA huduma zitolewazo kwa wateja wa NMB
waliojisajili kutumia NMB Mobile .Huduma inayomuwezesha mteja kupata huduma za kibenki
mahala popote bila kufika kwenye tawi la NMB.
Na Mwandishi Wetu
NMB imeendelea kuboresha huduma zake kwa kuzindua bidhaa na huduma mbali mbali ili kuwawezesha wateja kupata huduma za kibenki kwa urahisi na unafuu zaidi.
Na Mwandishi Wetu
NMB imeendelea kuboresha huduma zake kwa kuzindua bidhaa na huduma mbali mbali ili kuwawezesha wateja kupata huduma za kibenki kwa urahisi na unafuu zaidi.
Ili kukuwezesha kupata huduma za kibenki haraka na kwa wakati
wowote, Benki ya NMB imeendelea kuelemisha wateja wake aina mbalimbali ya
huduma za kibenki wanazoweza kuzipata bila ya kwenda katika tawi la NMB kupitia
kampeni yake maalum iitwayo JISEVIE.
Huduma zilizojumuishwa katika mpango huu maalum wa Jisevie ni
pamoja na Huduma ya NMB mobile, Huduma ya NMB PesaFasta, Huduma ya NMB ATM na
huduma ya kuweka na kutoa fedha kupitia Vodacom Mpesa.
“ Mpango huu wa kuelemisha wateja juu ya huduma mbali mbali
wanazoweza kuzipata bila ya kupitia benki, yaani Jisevie unalenga katika
kuendelea kutoa huduma bora zaidi , kuvutia na za haraka zaidi wakati wowote
mteja anapohitaji huduma za kibenki”, alisema bwana Arjan Molenkamp, Afisa Mkuu
wa Biashara ya Wateja Binafsi.
Wateja ambao wataweza kutumia moja ya huduma hizi zilizoainishwa
katika mpango huu wa Jisevie watapata faida mbalimbali ikiwemo; kutokutumia
fedha taslimu kulipia huduma mbali mbali, kuweka au kutoa fedha mahali popote
kwa kutumia huduma ya Vodacom Mpesa, Kutuma fedha kwa mtu yeyote asiye na
akaunti wala kadi ya ATM ya NMB kwa kutumia NMB PesaFasta na kutohitaji
kutembelea tawi lolote la benki ya NMB ili kuweka fedha kwenye akaunti yako.
Wateja wa NMB sasa wanaweza kupata huduma za kibenki popote walipo
bila kutembelea tawi la NMB. Haya yote yametokana NMB Jisavie ambayo
itamwezesha mteja wa NMB kuwa na NMB Mobile,NMB Pesa Fasta ,POS,NMB
ATM,Huduma ya kuweka na kutoa fedha kutoka kwenye akaunti ya NMB kwenda
M-Pesa na M-Pesa kwenda Akaunti ya NMB,Zaidi ya hayo yote NMB inalenga
kumuwezesha Mteja wake aweze kujihudumia mwenyewe bila kufika kwenye tawi la
NMB.
Faida nyingine anazoweza kupata Mteja wa NMB kwa kupitia mpango
huu wa Jisevie ni pamoja na kuangalia salio la akaunti yako, kupata taarifa
fupi ya matumizi ya akaunti yako, kununua Luku,Kulipa ankra ya Maji-DAWASCO,
kulipia bili ya King’amuzi ya DStv, Kulipia kodi za Mapato na kununua muda wa
hewani.
No comments:
Post a Comment