Waziri mkuu mstaafu, Mh. Frederick Sumaye akizungumza kwenye
sherehe za mahafali ya sita ya wahitimu 1029 wa chuo cha ualimu mjini
Singida. Kulia ni kaimu mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya ya
Singida, mwalimu Queen Mlozi na kushoto ni mmiliki wa chuo cha ualimu
Singida, Martin Makuza.
Mkurugenzi mtendaji wa Prime Education Network (PEN) Tanzaia,
Martini Mkauza akitoa nasaha zake kwenye sherehe za mahafali ya sita ya
chuo cha ualimu cha Singida mjini. Kulia ni waziri mkuu
mstaafu,Frederick Sumaye.
Waziri mkuu mstaafu, Mh.Frederick Sumaye akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu 1,029 wa chuo cha ualimu Singida.
Baadhi ya wahitimu wa chuo cha ualimu Singida,wakifuatilia kwa
makini hotuba ya waziri mkuu mstaafu Mh. Frederick Sumaye (hayupo kwenye
picha) wakati akizungumza kwenye sherehe za mahafali ya sita ya chuo
hicho.
Kikundi cha uhamasishaji cha kijiji cha Manguanjuki manispaa ya
Singida kikitoa burudani kwenye sherehe za mahafali ya sita ya chuo cha
ualimu mjini Singida.
Mmoja wa waandishi wa habari,Damiano Mkumbo akiwajibika kupata
picha safi kwenye sherehe za mahafali ya sita ya chuo cha ualimu mjini
Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu
Waziri Mkuu mstaafu Ferderick Sumaye amewataka wahitimu wa vyuo
vya ualimu wakatimize wajibu wao wa kufundisha kwa bidii na kuwalea
vizuri watoto watakaokabidhiwa ili wawe raia wema wa baadaye.
Akizungumza kwenye mahafali ya sita ya chuo cha ualimu Singida
kilichopo Singida mjini Sumaye ametoa changamoto hiyo akisema malezi ya
walimu yakiwa mema yatatuzalishia Watanzania wa kesho ambao rushwa kwao
itakuwa ni sumu inayonuka na ufisadi hautapata nafasi katika nchi yetu
na pia madawa ya kulevya hayataingizwa nchini na maovu yote yatatoweka
katika jamii.
Akifafanua zaidi, amesema walimu ndiyo wenye turufu ya kuamua ni Watanzania wa aina gani tunataka kuwatengeneza.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu huyo mstaafu ametumia fursa
hiyo kuwahakikishia wahitimu hao 1,029 kuwa pamoja na mapungufu mengi
yanayojitokeza, lakini serikali inajali sana maslahi ya walimu.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Prime Edecation Network (PEN)
Tanzania Martin Makuza, ameyaomba mashirika likiwemo la NSSF, kuangalia
uwezekano wa kuanza kuwakopesha wanafunzi wa ualimu kwa madai kwamba
wanafunzi hao kwa asilimia kubwa, wana uhakika wa kupata kazi na hivyo
kuwa na uwezo wa kurejesha mikopo.
No comments:
Post a Comment