Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, June 14, 2013

PICHA ZA MAMA ALIYEKAA JUU YA PAA KWA SIKU TANO KUZUIA NYUMBA YAKE KUUZWA NA BENKI YA TIB


Huyu mama alikaa juu ya paa kwa siku tano  tangu jumamosi kupinga nyumba yao kuchukuliwa na bank.Anasema mumewe alimdhamini mtu ambaye  alichukua mkopo bank miaka mingi iliyopita na kushindwa kulipa mkopo huo.
 Kwa mujibu wa maelezo yake , kesi yao bado ipo mahakamani kwani tayari yule mdaiwa kuna mali zake zilizotaifishwa.
Mdaiwa alikopa ml 240,  wameuza nyumba zake 2 na mabasi mawili.Wadaiwa  wanaomba kujua  kiasi kilichobaki  katika hilo deni  ili  watoe   na  kuuza  nyumba  yao.
Nyumba ipo mbezi Tangi bovu na inaeneo kubwa sana .Mama anasema hata akiuza si chini ya ml 500 iweje atolewe kwa ml 240  wakati mdaiwa nyumba zake mbili zimeshachukuliwa na mabasi mawili yale makubwa ya safari za mikoani  yamechukuliwa .Hiyo ml 240 haijatimia tu?na kama bado kiasi gani kimebaki?

 Ndani ya nyumba vitu walishachukua hao watu wa auction mart,   ndani kweupe.Na wakati haya yakiendelea hakukuwa na amri yoyote iliyotoka mahakamani wala hawakuwa na kibali cha mahakama.
Gea alimfuata huko huko juu kumsikiliza...
 Chumba cha habari cha clouds fm kinafuatilia  hapo bank ya Tanzania Investment bank(TIB) kujua chanzo  cha  tatizo maana wakati haya yakiendelea hiyo jana inasemekana hii nyumba ilikuwa  imeshauzwa.

Jana hiyohiyo,  mume wa huyu mama alikuwa mahakamani maana ilikuwa siku ya kesi kuendelea kusikilizwa. 

Taarifa  zinadai  kuwa Mumewe alirudi na oda maalum kutoka mahakamani kuwa nyumba hiyo isiguswe na vitu vyao virudishwe.

Dinamarios  Blog

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...