Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, July 12, 2016

MABONDIA KUPIMA UZITO IUMAA KWA AJILI YA KUCHEZA JULAI 16 TRAVELTAIN MAGOMENI


BONDIA Idd Mkwela ambaye yupo katika kambi ya Super D Coach Uhuru GYM Kariakoo amesema yupo tayali kupambana na bondia yoyote nchini kwa kuwa kapikwa na kuwa fiti zaidi kwa mazoezi anayopewa na kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kwa sasa yupo tayari kabisa kwa ajili ya mpambano wake ujao dhidi ya Hussein Gobos mpambano wa raundi sita kg 63 utakaofanyika julai 16 katika ukumbi wa Traveltain Hotel Magomeni Dar es salaam

Mkwela ambaye mpaka sasa amecheza mapambano matatu n katika hayo matatu ameshinda mawili kwa K,O na moja kutoka droo na katika mpambano wake wa mwisho alimsambalatisha Nassoro Madimb kwa K,O ya raundi ya pili mpambano wake ujao atakumbana na Gobos mpambano ambao unatolewa macho na mashabiki mbalimbali wa mchezo wa masumbwi nchini

mabondia hawo watakuwa wakisindikiza mpambano wa Hussein Itaba dhidi ya Ibrahimu Tamba
mpambano ambao umevuta hisia za mashabiki wengi wa kitongoji cha manzse na majirani wa maeneo hayo

mapambano mengine yatawakutanisha Juma Fundi atakaemkabili Said Chino katika mpambano wa raundi sita KG 54 na Ibrahimu Pazi atavaanana Sweet Kalulu katika mpambano wao wa KG 71wakati Emanuel Amosi atakumbana na Adam Kipenga


Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha  'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...