Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, July 12, 2016

TASWA QUEENS WAONDOKA NA MAKOMBE MAADHIMISHO YA SIKU YA WAANDISHI WA HABARI DUNIANI, JIJINI NAIROBI KENYA


 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Nchini Kenya, SJAK, Mbais Criss, akimkabidhi zawadi ya Kombe la mchezaji bora  Nahodha wa timu ya TASWA QUEENS, Lightness Sirikwa Mayeye, baada ya kutangazwa mchezaji bora aliyejituma katika mchezo wao dhidi ya timu ya SJAK ya Kenya.

Timu hizo zilizoshiriki katika Bonanza maalumu la Maadhimisho ya Siku ya Waandishi wa Habari Duniani, lililofanyika kwenye Uwanja wa Luna Park Jijini Nairobi Kenya Leo Julai 9, 2016,  zilitoka sare ya 0-0 katika muda wa kawaida na kupigiana penati ambapo Taswa Queens waliibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 4-3. Picha na Mafoto Blog
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Nchini Kenya, SJAK, Mbais Criss, akimkabidhi Kombe la ushindi Kipa wa timu ya TASWA QUEENS, Somoe Ng'itu, baada ya timu hiyo kuifunga timu ya SJAK ya Kenya kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya timu hizo kutoka sare ya 0-0 katika muda wa kawaida. 

Timu hizo zilishiriki kwa pamoja katika Bonanza maalumu la Maadhimisho ya Siku ya Waandishi wa Habari Duniani, lililofanyika kwenye Uwanja wa Luna Park Jijini Nairobi Kenya Leo Julai 9, 2016.
Kiungo wa timu ya Taswa Queens,  Ester Zelamula (kulia) akimtoka mchezaji wa Sjak ya Kenya, Mercy Njue, wakati wa mchezo wa kirafiki katika Maadhimisho ya Siku ya Waandishi wa Habari Duniani, uliochezwa kwenye Uwanja wa Luna Park Jijini Nairobi Kenya Leo Julai 9, 2016. Katikati ni Lightness Sirikwa wa Taswa Queens akijiandaa kutoa msaada.
 Kiungo wa timu ya Taswa Queens,  Ester Zelamula (kulia) akimtoka mchezaji wa Sjak ya Kenya, Mercy Njue, (katikati) Kushoto ni Lightness Sirikwa wa Taswa Queens akijiandaa kutoa msaada.
 Zelamula akiambaa na mpira baada ya mtoka Mercy Njue..
 Winga wa Taswa Queens, Angela Msangi (kulia) akipiga shuti huku beki wa Sjak ya Kenya, Rebecca Magoma, akijaribu kumdhibiti bila mafanikio.
 Lightness (kulia) akichuana kuwania mpira na Mercy.....
 Kipa wa Tswa Queens, Somoe Ng'itu akituliza mpira wakati wa mechi hiyo
 Lightness akiambaa na mpira.....
 Mtanange wa Taswa Fc dhidi ya Sjak ya Kenya ukiendelea. Katika mchezo huo Sjak waliibuka na ushindi.
 Mshike mshike langoni mwa Sjak....
 Julius Kihampa (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Sjak.......
 Khadija Kalili wa Taswa Queens (katikati) akimdhibiti Eveline wa Sjak....
 Angela Msangi akipiga shuti..........
 Angela Msangi akichuana kuwania mpira na beki wa Sjak Rebecca Magoma
 Ester Zeamula akifunga penati......
 Kipa wa Taswa Queens Somoe Ng'itu akiokoa penati ya Eveline....
 Kipa wa Taswa akibebwa juu kwa furaha baada ya kuokoa penati moja iliyowawezesha kuibuka kidedea.
 Picha ya pamoja kabla ya kuanza mechi hizo..
 Mazoezi ya kupiga danadana kabla ya mchezo wao...
 Katibu wa Chama cha Waandoshi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa) Amir Mhando akizungumza na wachezaji wa Taswa kabla ya kuanza kwa michezo hiyo.
 Picha ya pamoja
 Picha ya pamoja...

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...